رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا ۖ إِنَّكَ أَنتَ
السَّمِيعُ الْعَلِيمُ [٢:١٢٧]
Ewe
Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi [al-Baqarah
2:127]
رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن
ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ
عَلَيْنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ [٢:١٢٨]
Ewe
Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa
vizazi vyetu wawe umma ulio silimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na
utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. [al-Baqarah
2:128]
رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي
الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ [٢:٢٠١]
Mola
wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde na adhabu ya Moto!
[al-Baqarah 2:201]
رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَثَبِّتْ
أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ [٢:٢٥٠]
Mola
wetu Mlezi! Tumiminie subira, na isimamishe imara miguu yetu, na utusaidie
tuwashinde watu Makafiri [al-Baqarah 2:250]
رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ
أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ
عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا
طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ
أَنتَ مَوْلَانَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ [٢:٢٨٦]
Mola
wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe
mzigo kama  ulio wabebesha wale walio kuwa
kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na
utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde
kaumu ya makafiri [al-Baqarah 2:286]
رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ
هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ
[٣:٨]
Mola
wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kwisha tuongoa, na utupe rehema
itokayo kwako. Hakika Wewe ndiye Mpaji [Aal ‘Imraan 3:8]
رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً
طَيِّبَةً ۖ إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ [٣:٣٨]
Mola
wangu Mlezi! Nipe kutoka kwako uzao mwema. Wewe ndiye unaye sikia maombi. [Aal
‘Imraan 3:38]
رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا
وَإِسْرَافَنَا فِي أَمْرِنَا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ
الْكَافِرِينَ [٣:١٤٧]
Mola
wetu Mlezi! Tughufirie madhambi yetu na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu,
na isimamishe imara miguu yetu na utunusuru tuwashinde kaumu ya makafiri. [Aal
‘Imraan 3:147]
رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ
تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ [٧:٢٣]
Mola
wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama  hutusamehe
na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika. [al-A’raaf 7:23]
رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا مَعَ الْقَوْمِ
الظَّالِمِينَ [٧:٤٧]
Mola
Mlezi wetu! Usitujaalie kuwa pamoja na madhalimu (watu walio dhulumu.)
[al-A’raaf 7:47]
رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلْقَوْمِ
الظَّالِمِينَ [١٠:٨٥]
Ewe
Mola wetu Mlezi! Usitufanye wenye kutiwa misukosuko na hao watu madhaalimu.
[Yoonus 10:85]
وَنَجِّنَا بِرَحْمَتِكَ مِنَ الْقَوْمِ
الْكَافِرِينَ [١٠:٨٦]
Na
utuokoe kwa rehema yako kutokana watu makafiri. [Yoonus 10:86]
رَبَّنَا آتِنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً وَهَيِّئْ
لَنَا مِنْ أَمْرِنَا رَشَدًا [١٨:١٠]
Mola
wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uwongofu katika jambo
letu. [al-Kahf 18:10]
رَبِّ اجْعَلْنِي مُقِيمَ الصَّلَاةِ وَمِن
ذُرِّيَّتِي ۚ رَبَّنَا وَتَقَبَّلْ دُعَاءِ [١٤:٤٠]
Mola
wangu Mlezi! Nijaalie niwe mwenye kushika Sala, na katika dhuriya zangu pia.
Ewe Mola wetu Mlezi, na ipokee dua yangu. [Ibraaheem 14:40]
قَالَ رَبِّ اشْرَحْ لِي صَدْرِي [٢٠:٢٥]
وَيَسِّرْ لِي أَمْرِي [٢٠:٢٦]
وَاحْلُلْ عُقْدَةً مِّن لِّسَانِي [٢٠:٢٧]
Ewe
Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu,
Na
unifanyie nyepesi kazi yangu,
Na
ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu 
[Ta-Ha
20:25-27]
رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا [٢٠:١١٤]
Mola
wangu Mlezi! Nizidishie ilimu [Ta-Ha 20:114]
لَّا إِلَٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي
كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ [٢١:٨٧]
Hapana
mungu isipo kuwa Wewe Subhanaka Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni
mwa wenye kudhulumu. [al-Anbiya’ 21:87]
رَّبِّ أَنزِلْنِي مُنزَلًا مُّبَارَكًا وَأَنتَ
خَيْرُ الْمُنزِلِينَ [٢٣:٢٩]
Mola
wangu Mlezi! Niteremshe mteremsho wenye baraka, na Wewe ni Mbora wa
wateremshaji. [al-Mu’minoon 23:29]
رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَاتِ
الشَّيَاطِينِ [٢٣:٩٧]
Mola
wangu Mlezi! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashet'ani. [al-Mu’minoon 23:97]
وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحْضُرُونِ [٢٣:٩٨]
Mola
wangu Mlezi, wasinikaribie. [al-Mu’minoon 23:98]
رَبِّ هَبْ لِي حُكْمًا وَأَلْحِقْنِي
بِالصَّالِحِينَ [٢٦:٨٣]
Mola
wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema. [al-Shu’ara’
26:83]
رَبِّ نَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ
[٢٨:٢١]
Mola
wangu Mlezi! Niokoe na watu madhaalimu. [al-Qasas 28:21]
رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا
وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا [٢٥:٧٤]
Mola wetu
Mlezi! Tupe katika wake zetu na wenetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe
waongozi kwa wachamngu. [al-Furqaan 25:74]
رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ
الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا
تَرْضَاهُ وَأَدْخِلْنِي بِرَحْمَتِكَ فِي عِبَادِكَ الصَّالِحِينَ [٢٧:١٩]
Ee Mola
wangu Mlezi! Nizindue niishukuru neema yako uliyo nineemesha mimi na wazazi
wangu, na nipate kutenda mema uyapendayo, na uniingize kwa rehema yako katika
waja wako wema. [al-Naml 27:19]
رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ
جَهَنَّمَ ۖ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا [٢٥:٦٥]
Mola
wetu Mlezi! Tuondolee adhabu ya Jahannamu. Hakika adhabu yake ikimpata mtu
haimwachi. [al-Furqaan 25:65]

No comments:
Post a Comment