AFYA

Maajabu ya chumvi

Stori kuhusu chumvi:

Tunapata chumvi nyingi kwenye vyakula vyetu siku hizi. Chumvi nyingi itasababisha shinikizo la damu, uvimbe, matatizo kwenye kibofu cha mkojo, matatizo ya moyo na orodha inaendelea.
Tunaambiwa chakula chenye chumvi kidogo au kisicho na chumvi kabisa ndicho bora kwa afya zetu.

Ukweli kuhusu chumvi:

Mpaka zama za pili za mawe (middle stone ages), hakuna chumvi iliyokuwa mbaya. Waharifu waliuliwa gerezani kwa kupewa chakula bila chumvi, iliwasababishia kifo cha taratibu.
Miaka 2000 iliyopita, chumvi ilitumika kama hela. Dhahabu na Chumvi vyote vilikuwa na thamani sawa. Neno ‘salary’ (mshahara) linatokana na neno ‘salt’ (chumvi).
Hapa kwetu Tanzania, watu hutumia msemo, ‘Nimekula chumvi nyingi’ kumaanisha kuishi miaka mingi.
Katika siku hizo za kale, chumvi ilitumika pia kuhifadhia vyakula. Siku hizi tunatumia rifrijereta, kwa hiyo chumvi chache inahitajiwa isipokuwa kwa matumizi machache ya kusokotea nyama.
Wanyama wote wenye damu moto, lazima wawe na chumvi ili kuishi. Ubongo wa binadamu pamoja na uti wa mgongo, vimo katika mfuko wa maji chumvi uitwao ‘cerebrospinal fluid (csf)’. Umajimaji huu huzunguka sehemu zote za ubongo na uti wa mgongo.
Sote tulitumia miezi tisa kuishi katika mifuko ya uzazi ya mama zetu inayoelea kwenye maji chumvi (amniotic fluid).
Machozi yetu ni chumvi na tunatokwa na jasho ambalo pia ni chumvi. Mifupa yetu ina uwazi katikati yake (uboho) ambamo seli za damu hutengenezwa. Uboho huu umefunikwa na tabaka nyingi za chumvi kalisiamu kama vile kamba inavyoshikizwa pamoja. Kowa chumvi (salt crystals) zinashikizwa pamoja na kalisiamu, na kowa hizi ndizo zinazoifanya mifupa yetu kuwa imara, na siyo kalisiamu pekee.
Mifupa inamiliki asilimia 27 ya chumvi yote mwilini. Wakati mwili unahitaji chumvi zaidi, huikopa toka mifupani, jambo hili likitokea, kalisiamu huondolewa pamoja na chumvi na kuifanya mifupa kuwa miembamba, laini na midhaifu.
Chumvi imeundwa kwa Sodiamu na Klorini, kwa pamoja inaitwa; ‘Sodiamu kloridi’ (Na Ci).
Sodiamu ni metali laini yenye chaji chanya (+), wakati Klorini ni gesi yenye chaji hasi (-) ambayo hubadilika kuwa katika hali ya umajimaji inapoongezewa shinikizo.
Klorini ni gesi au umajimaji, lakini kwa namna fulani wakati dunia imeumbwa, klorini ilibadilika kuwa ngumu pamoja na sodiamu na madini mengine. Unaweza kuisaga chumvi na kuwa katika unga, klorini bado itabaki na sodiamu.
Klorini katika hali ya ugumuugumu, huitwa Kloridi.
Chumvi tutumiayo siku hizi inatoka katika bahari, maziwa, mito au katika migodi ya chumvi. Zaidi ya sodiamu na klorini, chumvi yote kwenye sayari yetu huja pamoja na madini mengine zaidi ya 80 ndani yake!.
Kwa hiyo tunaweza kuona ni jinsi gani madini hayo yalivyo na umhimu kwetu, la sivyo yasingeshikamanishwa na chumvi. Kwa sababu ya thamani yake kibiashara, madini hayo huondolewa ili kutengeneza faida kubwa.
Mwili wa binadamu una uwezo wa kuienguwa klorini kutoka katika sodiamu kadiri inavyohitajika. Damu yetu huihitaji klorini kama zifanyavyo ogani zingine ndani ya miili yetu.
Tumbo huitumia klorini kutengeneza haidrokloriki asidi inayohitajika ili kuuwezesha mfumo wa umeng’enyaji chakula kufanya kazi vizuri.
Miili yetu pia huitumia sodiamu kloridi kama chumvi kuufanya ubongo, uti wa mgongo, machozi, mifupa, tezi za jasho, ogani na damu kufunikwa na chumvi.
Mwili unanufaika pia kutoka katika madini mengine yaliyomo katika chumvi ili kuuweka katika hali ya ualikalini na afya.
Ni kama na vile kwa kunywa maji kuzidi kunaweza kumuua mtu (hyponatremia), vivyo hivyo kwa kutumia chumvi kuzidi, kunaweza sababisha; uvimbe, kuharisha na kifo.
Chumvi ya mezani husafishwa kwa kuondoa madini madini na hupitishwa katika joto la nyuzi joto 1093. Kwa hiyo uliyonayo sasa ni asilimia 40 ya sodiamu na asilimia 60 ya kloridi, na kisha kemikali kama vile ‘aluminium silicate’ huongezwa ili kuifanya isishikane na hivyo kubaki katika hali ya unga. Aluminium silicate ni sumu kali inayoharibu mfumo wetu wa fahamu. Inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Sodiamu iliyozidi inaweza kutokea kutokana na kula vyakula vingi vyenye viongezi (additives) vya sodiamu. Sodiamu siyo chumvi, chumvi ni sodiamu-kloridi. Sodiamu bikaboneti, sodiamu benzoeti na monosodiamu glutameti (msg) ni baadhi ya viongezi hivyo.
Sodiamu, potasiamu na kloridi ni elektrolaiti (madini maalumu) ambayo huyeyuka katika maji na kubeba chaji za kiumeme na kuzipeleka sehemu zozote za mwili kuliko na maji. Madini haya yenye chaji za kiumeme yana uwezo wa kuingia na kutoka ndani ya seli kwa uhuru wote, huku yakipeleka lishe ndani na kubeba nje taka na maji yaliyozidi ili kuiacha seli katika hali yake ya usawa (balanced cell).
Wakati huo huo, kadiri elektrolaiti hizi zikitembea ndani na nje ya seli na kufanya mabadiliko yake, usawa maalumu wa Potasiamu ndani ya seli lazima utunzwe kwa kiasi maalumu cha sodiamu na kloridi ili kuishikilia potasiamu ndani katikati ya seli.
Elektrolaiti zinapatikana kwenye majimaji yote mwilini na hubeba mapigo (impulses) kwenye neva zetu. Kitendo hiki huusaidia moyo na kiwambo cha moyo (diaphragm) kusinyaa na kulegea.
Elektrolaiti hubeba Glukozi (damu yenye sukari) na kuipeleka ndani ya seli baada ya Insulini kufungua milango kwa ajili ya sukari kuchukuliwa.
Elektrolaiti pia huwasha pampu za kuzarishia nguvu ziitwazo kwa kitaalamu ‘Cation pumps’ ambazo huzarisha umeme ambao huifadhiwa kwenye beteri zijulikanazo kwa kitaalamu kama ‘mg Adenosine Triphosphate (mgATP)’ na ‘mg Guanosine Triphosphate (mgGTP)’ za mwili.
Ikiwa mtu atapungukiwa kwa kiasi kingi cha Elektrolaiti hizi kutokana na kuharisha au kwa sababu ya dawa za kukojosha (diuretics), anaweza kuwa mgonjwa sana na itamlazimu kwenda hospitali kupewa elektrolaiti hizi katika mfumo wa dripu (intraveneous fluid, IV), kama vile; maji chumvi (saline solution), maji sukari (dextrose fluid) na madini.
Siku hizi vinywaji vyetu vingi baridi vinaongezwa kafeina ambayo ni kikojoshi kinachoyalazimisha maji kutoka ndani ya mwili na kutusababishia upungufu wa maji mwilini (dehydration).
Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj, hakuna kinywaji ambacho ni mubadala wa maji.
Wanasayansi na madaktari bado hawaelewi ni kwa jinsi gani chumvi huyeyuka ndani ya maji au ni kwa vipi iwezavyo kuendelea kuwa na hali ya uchumvi na uchumvi. Wanasayansi na wanakemia wana baadhi za nadharia, lakini bado hawajaweza kuzithibitisha. Bado imebaki kuwa ni fumbo (mystery).

Baadhi ya kazi zingine mhimu za chumvi:

  • Chumvi huyalazimisha baadhi ya maji kubaki nje ya seli. Inarekebisha uwiano sawa wa kiasi cha maji yaliyopo nje ya seli. kuna bahari mbili za maji ndani ya mwili, bahari moja imejishikiza NDANI ya seli, na bahari nyingine ya pili imejishikiza NJE ya seli. Afya bora inategemea uwiano mzuri wa ujazo wa maji uliopo baina ya bahari hizi mbili, na usawa huu unawezeshwa pekee na chumvi, chumvi ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi.
  • Chumvi husaidia kuondoa dalili za mfadhaiko (stress).
  • Figo hazitaweza kufanya kazi zake vizuri bila chumvi.
  • Kukata tamaa na matatizo ya kisaikolojia, vitaondolewa kwa kuchukuwa chumvi zaidi, kula mlo kamili na kufanya mazoezi ya kutembea.
  • Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida yanaweza kurudishwa katika hali yake ya kawaida kwa kuchukuwa kipande cha chumvi na kukiweka mwishoni mwa ulimi na kukifanya kiyeyuke.
  • Mifupa inapata uimara wake toka katika chumvi, na siyo katika kalisiamu pekee.
  • Je wewe ni mwanaume na unashindwa kuhimili kusimama? unahitaji chumvi zaidi na kunywa maji halisi zaidi.
  • Kuichukuwa chumvi na kunywa maji kabla ya mazoezi, kutakusaidia kupumua vizuri na kutokwa na jasho chache.
  • Matatizo ya kibofu cha mkojo na upotevu wa mkojo wa makusudi, vingeweza kurekebishwa kwa kuongeza chumvi zaidi kwenye mlo wako.
  • Dalili za maumivu ya jongo (Gout) zinaweza kuzuiwa kwa kutumia chumvi.
  • Chumvi ni mhimu ili kuzuia kuvimba kwa mishipa na vena kwenye miguu.
  • Kwa sababu tunapata potasiamu karibu katika kila chakula tunachokula, chumvi inatakiwa kuongezwa katika milo yetu, hii itairuhusu miili yetu kuhimili usawa sahihi wa maji kati ya bahari ya ndani na ile ya nje ya seli.
  • Chumvi ni mhimu ili kuondoa asidi iliyozidi kwenye seli, hasa seli za ubongo.
  • Chumvi ni mhimu kwa ajili ya kusawazisha kiasi cha sukari kwenye damu, hivyo kuzuia ugonjwa wa kisukari.
  • Chumvi ni mhimu katika uzarishaji wa nguvu umeme itokanayo na maji katika seli zote za mwili.
  • Chumvi ni mhimu katika mawasiliano ya neva na ufanikishwaji wa taarifa wakati wote seli za ubongo zinapofanya kazi tangu kuzaliwa hadi kufa.
  • Chumvi ni mhimu katika umeng’enywaji wa chakula na madini kwenye utumbo mdogo (intestinal tract).
  • Chumvi ni mdhibiti madhubuti dhidi ya histamini.
  • Chumvi ni mhimu ili kuzuia mikakamao ya mishipa (cramps).
  • Chumvi ni mhimu katika kusafisha makohozi na kubana kwa kifua.
  • Chumvi ni mhimu ili kuzuia uzarishaji wa kuzidi wa mate katika kiwango kwamba yanatoka nje ya mdomo wakati umelala, kitendo hiki cha kutoa mate (udenda) wakati umelala ni dalili ya upungufu wa chumvi mwilini.
  • Chumvi ina umhimu mubwa katika uimarishaji wa mifupa. Ugonjwa wa mifupa (osteoporosis) kwa sehemu kubwa, ni matokeo ya upungufu wa chumvi na maji mwilini.
  • Chumvi ni mhimu katika usafishaji wa makohozi mapafuni na maji yaliyogandamana hasa kwa watu wenye pumu, ikiwa inakulazimu kusafisha koo kila wakati, ni dalili kuwa umepungukiwa chumvi.

Chumvi kiasi gani?

Dr.Batmanghelidj anashauri; ¾ (robotatu) gramu za chumvi kwa kila nusu lita ya maji (16 ounces), au nusu kijiko cha chakula kwa kila nusu galoni ya maji, au kijiko kimoja cha chakula kwa kila galoni moja la maji tunayokunywa. Hiki ni kiasi kizuri kwa kuanzia na siyo kanuni, tafadhari tumia aina ya kijiko kilichotajwa hapo juu kwa vipimo sahihi.
Ukiona viwiko, vidole au kope za macho zinavimba, usitumie chumvi kwa siku 2, kunywa maji halisi pekee na kisha siku ya tatu, endelea kuchukuwa chumvi tena.

Namna bora za kula chumvi:

  • Njia ya kwanza ni kuiweka chumvi katika sehemu ya mbele ya ulimi, hakikisha unaihisi radha yake, na kisha kunywa maji juu yake yakiisafisha kuelekea chini.
  • Unaweza pia kuongeza chumvi ya ziada kwenye chakula chako.Tatizo la njia hii ni kuwa, chakula kinahisika kuwa na chumvi zaidi ya radha zingine.
  • Unaweza pia kunywa nusu ya maji unayotaka kunywa, kisha utamung’unya taratibu chumvi mdomoni kama ulavyo pipi, na kisha umalizie nusu ya maji iliyobaki.
  • kuichanganya chumvi pamoja na maji ya kunywa si wazo zuri sana.
Mhimu: Tumesema chumvi ya mawe ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi sababu ya madini madini mengine zaidi ya 80 yaliyomo ndani yake, lakini hatuwezi kubeza umhimu wa madini joto (iodine) kwa afya ya mwili, ikiwa ni hivyo basi, tunashauri kwa wale ambao hawana vyanzo vingine vya madini hayo ya joto kutumia chumvi zote mbili yaani robo tatu ya matumizi yawe chumvi ambayo haijasafishwa na robo nyingine iwe ile iliyosafishwa ili kuepuka kupungukiwa madini hayo mhimu. Tunasisitiza katika chumvi hiyo iliyosafishwa hakuna kingine kilicho mhimu zaidi ya madini hayo joto ambayo yanaweza kupatikana pia kwa kula vyakula vingi vya baharini (sea foods).

Jitibu kwa kutumia maji

Mambo ya kuzingatia kabla ya kuanza tiba kwa kutumia maji: 

Kanuni ya kimakisio kwa mahitaji ya maji ni; kunywa nusu ya uzito wako katika aunsi (ounces) ugawe mara mfululizo utakaoufuata kwa siku nzima. Kiasi kidogo chini au juu ya hiki, kinakubalika. Aunsi 1 = miligramu 31.25.
Kanuni ya kimakisio kwa mahitaji ya chumvi ni, Robo tatu gramu za chumvi kwa kila nusu lita ya maji, nusu kijiko cha chakula kwa kila nusu galoni ya maji au kijiko kimoja cha chakula kwa kila galoni moja la maji.
Pengine umeshageuza kichwa na kujisemea, “Wewe ni kichaa…..hicho ni kiasi kingi sana cha maji”. Ukweli ni kuwa, ni rahisi kunywa hivyo hasa tukitumia sentensi, glasi 8 za maji zikigawanywa mara nane kwa siku (glasi 1 = ml 250 au robo lita).

Mfano, kwa mtu mwenye uzito wa kilogramu 75:

  • Badili kilogramu kwenda aunsi kwa kuzidisha mara 2.2. Hivyo, 75×2.2 = aunsi 165.
  • Tafuta nusu ya aunsi kwa kugawa aunsi na 2. Hivyo, aunsi 165/2 = aunsi 82.5.
  • Gawanya mara mfululizo utakaoamua kuufuata kwa siku nzima, mfano mara 8 kwa siku. Kwa hiyo aunsi 82.5/8 = aunsi 10.3.
  • Badili aunsi kuwa miligramu za maji. Aunsi 1 = miligramu 31.25. Kwa hiyo aunsi 10.3×31.25 = miligramu 322.
Kwa hiyo itampasa mtu huyo mwenye uzito kilo 75, kunywa ml 322 za maji mara nane kwa siku.
Namna anavyopaswa kufuata hiyo ratiba mara 8 kwa siku:
1) Akiamka tu (mfano saa 12 kamili asubuhi), cha kwanza atakunywa maji ml 322. ataendelea na shughuli zake za asubuhi
2) Nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi (yaani saa 12:30 asubuhi), atakunywa maji ml 322. atasubiri nusu saa ipite ndipo atapata chakula chake cha asubuhi (itakuwa saa 1 kamili asubuhi).
3) Kisha kula chakula cha asubuhi, atahesabu masaa 2 na nusu ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 3 na nusu asubuhi).
4) Atahesabu masaa 2 tena ndipo atakunywa tena ml 322 nusu saa kabla ya chakula cha mchana (itakuwa saa 6 mchana) kwa hiyo nusu saa baadaye atakula chakula cha mchana (yaani saa 6 na nusu mchana).
5) Atahesabu yapite masaa 2 na nusu baada ya chakula cha mchana ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 9 kamili alasiri).
6) Atahesabu masaa 2 na nusu yapite ndipo atakunywa maji ml 322 nusu saa kabla ya chakula cha jioni (itakuwa saa 11 na nusu jioni). Nusu saa baadaye atakula chakula cha jioni (itakuwa saa 12 kamili jioni).
7) Kisha kula chakula cha jioni, atahesabu masaa 2 na nusu tena ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 2 na nusu usiku).
Muda wowote atakapokwenda kulala kuanzia saa 4 usiku atakunywa tena maji ml 322 kumalizia mara 8 zake kwa siku.
Huyo alikuwa na kilo 75, sasa na wewe andika uzito wako na utumie fomula hiyo hapo juu ujuwe ni kiasi gani cha maji unahitaji kwa siku na kisha ufuate mara hizo 8 kama zilivyopendekezwa hapo juu. Kwa staili hii ndipo maji huwa ni zaidi ya dawa.
Kila mmoja wetu sasa anaweza kutumia uzito wake kwa kutumia fomula hii na kujua ni kiasi gani cha maji anahitaji kwa siku.
Kumbuka, Kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi ni kiasi cha chini kabisa, lakini mahala pazuri pa kuanzia, ikiwa ni mtu unayejishughurisha zaidi na mazoezi au unaishi katika mazingira ya joto zaidi, utahitaji zaidi ya hapo.
Sasa, hutakubali kuwa kunywa maji kwa protokolo hii ni kazi rahisi?.
Ikiwa haunywi kiasi hiki cha maji kwa sasa, unapaswa kuanza kuongeza kiasi cha ziada kwa taratibu sana. Hii itaupa nafasi mwili kujirekebisha kuendana na kiasi ulichoanza kukiongeza, na ikiwa hautaupa mwili muda wa kujirekebisha, basi maji yatakuwa kama dawa ya kukojosha (diuretic), yakisukuma madini na vitamini za mhimu nje ya mwili, pengine na kukusababishia madhara zaidi kuliko faida.
Watu wazee na watoto wadogo wanatakiwa kuanza kuongeza maji kufikia mahitaji yao kwa taratibu zaidi.
Kwa kutumia mfano wa uzito hapo juu, itakupasa kuanza na glasi 3 siku ya kwanza huku ukiongeza glasi moja zaidi kila siku inayofuata mpaka ufikie glasi zote 8.
Kumbuka kuwa, kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi na kula chumvi robo tatu gramu kwa kila nusu lita ya maji, ni kanuni ya kimakisio tu. Baadhi ya wengine watahitaji maji zaidi wakati wengine watahitaji chumvi zaidi. Baada ya muda, mahitaji ya mwili kwa maji na chumvi yanaweza kuongezeka kidogo zaidi sababu ya mazingira ya joto, mazingira ya baridi au mazoezi ya viungo.
Kila mmoja lazima apate kujua kiasi cha mahitaji ya mwili wake kwa maji kuanzia sasa.
Kamwe usinywe zaidi ya aunsi 33.8 (lita moja) za maji kwa wakati mmoja ukiwa umekaa au umesimama.
Watoto wadogo kuanzia miaka 2 mpaka 12, hasa wale wepesi kujishughulisha na mazoezi wanahitaji asilimia 75 mpaka 100 za aunsi za maji katika uzito wao kwa sababu miili yao inakua muda wote na kila seli katika miili yao inayokua inayahitaji maji haya ya ziada (mytosis).
Tiba hii ya maji haitumiki kwa watoto chini ya miaka 2.
Chumvi ya kawaida ya mezani iliyoongezwa madini ya iodini, itakusaidia kidogo, chumvi ya mawe ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi sababu ya madini mengine mengi ya ziada zaidi ya 80 yaliyomo ndani yake. Chumvi ya baharini pia huwa na radha nzuri, nyeupe na umajimaji kidogo.

Namna bora za kula chumvi:

  • Njia ya kwanza ni kuiweka chumvi katika sehemu ya mbele ya ulimi, hakikisha unaihisi radha yake, na kisha kunywa maji juu yake yakiisafisha kuelekea chini.
  • Unaweza pia kuongeza chumvi ya ziada kwenye chakula chako.Tatizo la njia hii ni kuwa, chakula kinahisika kuwa na chumvi zaidi ya radha zingine.
Ukiona viwiko, vidole, miguu, mikono au kope za macho zinavimba (kuvimba kusikotokana na ajali au jeraha), au unaharisha zaidi, usitumie chumvi kwa siku 2 mpaka 3, kunywa maji halisi pekee na kisha siku ya tatu, endelea kuchukuwa chumvi tena, lakini ichukuliwe taratibu. Kamwe usitumie chumvi zaidi ya robo tatu gramu kwa kila nusu lita ya maji.
Kumbuka chumvi ikizidi hupelekea kuharisha.
Dr.Batmanghelidj anasema, kunywa maji matupu kunaweza pelekea mwili kupoteza baadhi ya madini na vitamini zake mhimu nje ya mwili na hivyo kutozipa seli muda wa kutosha kuyatumia maji. Inashauriwa kutumia vidonge vyenye vitamini nyingi kwa pamoja (multivitamins) katika kila mlo wako ili kurudishia kile kitakachokuwa kimepotea (hasa ikiwa haufanyi mazoezi na kula kiasi kingi cha mboga za majani).
Uvimbe utakapokuwa umepotea au umeacha kuharisha, unaweza kuendelea na mpango wako wa kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi ingawa mara hii utayachukua kwa kiasi kidogo.
Kwa siku nzima, anza kuongeza kiasi cha unywaji wako wa maji mpaka ufikie tena nusu ya uzito wako katika aunsi, anza pia kuchukua chumvi pamoja na maji. Unatakiwa kuhakikisha kuwa unapata gramu 150 za madini ya iodine kwenye “multivitamins” zako kila siku mpaka gramu 450 kwa siku.
Kisha kunywa maji, maji yanapaswa kubaki ndani ya mwili masaa 2 mpaka 2 na nusu ili kuupa mwili muda wa kutosha kuyatumia maji hayo vizuri.
Ikiwa inakulazimu kukojoa (peeing) chini ya muda wa masaa 2 tangu unywe maji, utalazimika kuacha kunywa maji matupu, jaribu kunywa juisi (uliyotengeneza mwenyewe) ya chungwa, ya limau au ya zabibu au juisi nyingine yeyote isipokuwa kwa watu wanaosumbuliwa na pumu (asthma) ambao hawatakiwi kunywa juisi ya chungwa.
Wakati huo huo mhimu kukumbuka kuongeza robo tatu gramu za chumvi katika kila nusu lita ya juisi yako.
Ikiwa kunywa juisi hakutasaidia kupunguza kwenda bafuni kila mara, jaribu kunywa maji huku ukila mkate. Unaweza kuongeza krimu ya siagi au jamu kwenye mkate wako (the magic bagel).
Kisha kutumia mkate siku moja au mbili unaweza kupunguza sasa kiasi cha mkate mpaka nusu yake, robo yake na mwisho juisi pekee pamoja na mlo wako.
Utapaswa kurudi taratibu tena kutoka kunywa maji juisi mpaka kunywa maji matupu tena, baada ya siku kadhaa itakupasa kujaribu aunsi 2 za maji matupu nusu saa kabla ya chakula, kesho yake aunsi 4, siku inayofuata itakuwa aunsi 6 kisha 8 na kuendelea mpaka ufikie kiasi chako unachotakiwa.
Ikiwa kunywa maji pamoja na kula mkate au katika juisi hakukusaidii kupunguza kwenda bafuni, Glasi ya maji (ml 250) matupu ikiongezwa na kijiko (kijiko cha chakula) kimoja cha asali au sukari halisi au walau sukari nyeupe kutakutatulia tatizo hili ukiongeza na chumvi 1/8 ya kijiko cha chai , tikisa na kisha kunywa mchanganyiko huo.
Bilashaka umewahi kusikia msemo, “Kwa sehemu kubwa tumetokana na maji”, hii ndiyo sababu zaidi ya asilimia 94 ya damu yetu ni maji, zaidi ya asilimia 85 ya ubongo wetu ni maji, huku zaidi ya asilimia 75 ya sisi ni maji.
Muda gani unywe maji:
Kitu cha kwanza kufanya mara uamkapo tu, ni kunywa glasi 2 za maji (ml 500) kwakuwa umetumia glasi 2 za maji kwa kulala mpaka asubuhi.
Kunywa glasi 1 robo saa au glasi 2 nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni, kisha hesabu masaa 2 au 2 na nusu kila baada ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni bila kunywa wala kula chochote, ndipo unywe glasi 1 ya maji.
Kunywa glasi 1 ya maji kila uendapo kulala.
Muda wowote uamkapo usiku kwenda bafuni, kunywa nusu glasi ya maji na kipande cha chumvi kisha rudi kulala.
Muda wowote unapopatwa na kiu kunywa maji.

Kwanini unywe maji robo lita, robo saa kabla ya kula, au nusu lita, nusu saa kabla ya kula?:

Wanyama wote hunywa maji halisi (plain water). Ikiwa utawachunguza paka na mbwa, mara zote hunywa maji na kusubiri wastani wa nusu saa kabla ya kula. Ratiba inabadilika wanapokuwa wanatibiwa, hapa hunywa na kisha hula papo hapo ama baadaye.
Mfululizo huu ni mhimu ili kubaki na afya bora.
Unapokunywa maji na kusubiri nusu saa kabla ya kula, maji yanaenda tumboni na kuziamsha tezi kutoa kemikali (homoni) kuzifunika kuta za tumbo ili kuzirinda dhidi ya haidrokloriki asidi ambayo huzarishwa wakati chakula kinawekwa mdomoni.
Maji na kemikali hizo kisha huenda kwenye utumbo mdogo ambako kemikali hizi hukaa kusubiri chakula kitakachokuwa kinakuja baadaye. Maji hayo huru, yanauacha utumbo mdogo na kwenda katika seli zote za mwili na kuzijaza (kuzinyweshea) maji kama vile unavyonywesha bustani. Baada ya seli kuwa      zimenyeshewa, maji yanayobaki kisha yanasukumwa tena kwenda tumboni ili kunyeshea chakula kilichofika.
Nguvu zetu hazitokani na vyakula tunavyokula, bali zinatoka katika maji ambayo yanaiweka atomu ya haidrojeni katika chakula.
Tunatembea katika haidrojeni.
Vyakula tulavyo hutupatia vitamini na madini tunayoyahitaji ili kubaki katika afya.
Ikiwa haunywi maji halisi (glasi 1 au 2) kabla ya kula chakula na kusubiri (robo saa au nusu saa), basi mwili lazima ujikope maji wenyewe!.
Kama mwili utakopa maji toka katika damu, basi ateri lazima zipunguze vipenyo vyake na moyo lazima utumie nguvu nyingi ili kusukuma damu ambayo ni nene (nyingi), kitendo hiki tunakiita ‘shinikizo la damu’(BP).
Ikiwa mwili utajikopa maji toka katika ubongo, utapatwa na ‘kichwa kizito’ au kichwa kuuma ambacho kinaweza pelekea maumivu ya kichwa.
Ikiwa unakunywa alikoholi (pombe) na inavuta maji toka kwenye ubongo, utapatwa na kutokujisikia vizuri au uchovu (hangover).
Watu wanaoishi katika nchi za baridi huweka alikoholi kwenye tenki zao za gesi ili kuvuta maji ndani ya gesi na hivyo kuifanya gesi isigande.
Kokote katika ogani au tishu mwili utakakokopa maji, lazima ogani au tishu hiyo iachiwe madhara na hivyo kusababisha maumivu ama ufanyaji kazi wa ogani au tishu hiyo usio wa kawaida kama vile kufunga choo (constipation).
kufunga choo au kupata choo kigumu sana kunatokea wakati mwili umekopa maji toka katika utumbo mdogo na sehemu ya chini ya utumbo mpana kunakopelekea taka za mwili kusimama kwenye kuta za utumbo mdogo na sehemu ya chini ya utumbo mpana (colon). Wakati mambo yako yanapokuwa na umajimaji, huteleza yenyewe chini bila kutumia nguvu yoyote.
Kila tunapopumuwa hewa nje (exhale) tunapoteza maji!.
Ikiwa utahema juu ya kioo, utauona ukungu (maji). Tunapoteza glasi 4 za maji kwa kupumuwa tu kila baada ya masaa 24!!.
kama mwili utakopa maji toka mapafuni, utapatwa na pumzi fupi itakayopelekea upatwe na pumu (asthima) na matatizo mengine yanayohusiana na mfumo wa upumuwaji.
Mapafu na Moyo vinauhusiano wa karibu, kwa hiyo kama mwili utakopa baadhi ya maji toka katika mishipa ya moyo, utapatwa na maumivu ya moyo ambayo yanaweza kurahisisha kutokea kwa shambulio la moyo (heart attack).
Mishipa inahitaji damu na maji wakati unafanya mazoezi, kwa hiyo kama unatakiwa kula chakula na kisha kutembea au kupandisha ngazi (za ghorofa) na una upungufu wa maji (dehydrated), unaweza ukapatwa na pumzi fupi, shambulio la pumu, utapatwa na maumivu ya moyo (angina) au kukakamaa kwa mishipa (cramps).
Ndiyo maana wanasema; kamwe usiende kuogelea mara tu baada ya kumaliza kula kwa sababu mishipa itakakamaa.
Mwili unapokuwa katika kazi yake ya umeng’enyaji chakula, huielekeza (diverts) damu toka katika mikono na miguu kwenda katika utumbo mdogo ili kusaidia umeng’enyaji wa chakula.
Baadhi ya vyakula ni rahisi kumeng’enywa na vinawezeshwa na maji pekee, kama vile matunda na mboga za majani.
Vinywaji vingine (liquid beverages) kama vile kahawa, chai, soda na juisi, siyo maji kwa mwili. Hivi ni vyakula pia kwa sababu ulimi unaipata radha ya viongezi (additives) na siyo radha ya maji halisi, na hivyo tumbo litaitowa haidrokloriki asidi. Mwili utakishughurikia kinywaji hicho kama chakula.
Utafaidika na baadhi ya maji kama vile katika matunda na mboga za majani kwa masharti ya kinywaji hicho kutokuwa na kafeina (caffeine).
Kafeina ni kikojoshi (diuretic), huyalazimisha maji kutoka nje ya mwili.
Magonjwa mengine yanayoweza kuepukika kwa kunywa maji kabla ya kula ni pamoja na vidonda vya tumbo, tumbo kunyonga, kiungulia, mafuta yaliyozidi, kansa ya utumbo mdogo, kukinaishwa na chakula, na ernia.
Kunywa maji masaa 2 au 2 na nusu baada ya chakula kunasaidia kumalizia umeng’enyaji wa chakula na kuunywesha mwili maji baada ya kukaukiwa kulikosababishwa na kazi ya umeng’enyaji wa chakula.
kunywa maji ya kawaida katika joto la kawaida.
Magonjwa mengine yanayotibika au kukingika kwa kutumia tiba ya maji ni; Kansa, kisukari, kifua kikuu (TB), shinikizo la damu(BP), mfadhaiko (stress), matatizo ya moyo na kuzimia, magonjwa ya tumbo, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya Ini, pumu (Asthima), mzio (Allergy), chunusi, homa, kupunguwa nguvu na kinga ya mwili, matatizo ya kina mama, magonjwa mengine ni pamoja na homa ya uti wa mgongo, kansa ya kizazi, kikohozi, kuharisha, kikundu, nyongo, matatizo ya tumbo, kupungua uzito, upungufu wa damu (anaemia), vichomi, vidonda vya tumbo, utipwatipwa, kuzeeka mapema, na magonjwa mengine mengi.
Tiba hii ni nzuri kwa wote, wagonjwa watapona na wazima watabaki na afya bora na kujirinda dhidi ya maradhi kwa maisha yao yote.
”Kuna maajabu zaidi ya milioni katika glasi moja ya maji kuliko katika dawa yeyote utakayoandikiwa na muuguzi wako – dr.Batmanghelidj”.

Angalizo:

  • Ikiwa hauendi chooni walau mara tatu kwa siku,unapaswa kumwona daktari kabla ya kuanza tiba hii.
  • Figo zako lazima ziwe zinafanya kazi vizuri, hii inamaanisha, kiasi cha maji unachokunywa lazima kiwe karibu sawa na unachotoa.
  • Wakati huo huo, kwenda chooni mara nyingi kwa siku kunaweza kukusababishia kupoteza vitamini mhimu, madini na elektrolaiti na kukufanya vibaya zaidi ya vizuri.
  • Unatakiwa kuwa makini sana unapoanza kuongeza uchukuaji wa maji mwilini, anza pole pole kwa kuongeza glasi 1 kila siku mpaka utakapofikia nusu ya uzito wako katika aunsi. lazima uupe mwili muda wa kujirekebisha baada ya kuzoea vinywaji kama kahawa, chai na soda, kwa kuwa vinywaji hivi huufanya mwili kujiendesha kwa namna nyingine.
  • Unaweza kuumwa na kichwa au unaweza usijisikie vizuri tu siku tatu mpaka wiki moja za kuanza tiba, usiache kunywa maji kwakuwa hayo si madhara bali ni dalili kuwa taka za sumu zimeanza kuondoka mwilini, baada ya muda utarudi katika hali yako ya kawaida.
  • Tunashauri watu wenye matatizo ya figo, Ini na moyo, kutofuata tiba hii mpaka watakapopata ruhusa ya daktari na muongozo sahihi.
  • Usinywe maji zaidi ya lita 3.78 kwa siku.
  • Usinywe maji kuanzia lita moja kwa pamoja au ukiwa umekaa katika mkao mmoja iwe kusimama au kukaa.
Kumbuka pia kuwa hii ni elimu tu na siyo kumuondoa daktari wako au chaguo lako la kutumia dawa, ni programu iliyopendekezwa kwa manufaa yako.

---------------------------------------------------------------------------------------
Kolesteroli au helemu ni nini? Ni dhahiri na rahisi kabisa, ni kama nta laini ambayo huelea katika damu na katika seli zako zote za mwili muda wote.  
Kwa baadhi ya watu kolesteroli ina mwelekeo wa kujilundika kwenye ateri karibu na moyo au shingoni. Ikiwa mkusanyiko huu wa kolesteroli unaendelea kuwa mwingi kiasi cha kuanza kuzifunga ateri, huweza kusababisha mishtuko au shambulio la moyo (heart attack).

Ukweli ni kuwa kolesteroli si mojawapo ya vitu ambavyo watu hupenda kujichunguza. Isitoshe mwili unaitengeneza kila siku ili kwamba unaweza kufurahi kuwa mzima. Ubongo umetengenezwa kwa kolesteroli, homoni zako zimetengenezwa kwa kolesteroli na hata neva zako zimefunikwa na kolesteroli (myelin sheaths). Bila kolesteroli huwezi kuishi.

Ikiwa kolesteroli ni kitu kibaya sana, kwanini Ini lako huizarisha kwa wingi kiasi hicho?:

Asilimia 75 ya kolesteroli katika damu hutengenezwa na Ini. Asilimia nyingine 25 hutujia toka kwa kile tunachokula. Kadiri ulavyo kolesteroli nyingi, ndivyo na Ini huitengeneza chache ili kukuweka wa furaha. Ini lako linatengeneza wastani wa mg 900 kwa siku. Kwa wastani, watu hula mpaka mg 300 za kolesteroli kwa siku. Ukichanganya pamoja, mtu wa kawaida ana mg 1200 za kolesteroli katika mfumo wake wakati wowote.

Kwanini katika maisha Ini letu litakuwa linatengeneza mg 900 za kolesteroli kila siku huku tunaambiwa chochote zaidi ya mg 200 ni hatari?, tunaweza kusema tu haileti maana (Nonesense).

Unapokula chakula chochote chenye kolesteroli, kolesteroli lazima iende kwanza katika kuta za tumbo kwa ajili ya kuingia kwenye mkondo wa damu.
Cha kushangaza ni kuwa tumbo (intestine) lina uwezo mdogo sana wa kuimeng’enya kolesteroli unayokula. Katika hali hii mwili wako ndio hasa hukulinda usipate kolesteroli nyingi kupitia chakula ulacho. Ikiwa itatokea umekula chakula ambacho kina kolesteroli nyingi, sehemu kubwa ya kolesteroli itatoka nje wakati unapata choo.

Hautapata ishara yeyote ya onyo kwamba una kolesteroli iliyozidi. Namna moja ya kutambua kwa hakika ni kufanya kipimo kiitwacho “lipoprotein profile” . kipimo hiki kitaonesha jumla ya kolesteroli uliyonayo, HDL cholesterol, LDL cholesterol na usawa wa triglyceride. Kipimo hufanyika baada ya kufunga masaa tisa mpaka kumi na mbili bila chakula, kimiminika au dawa.

Katika miaka ya 1970 kiasi kilichokuwa kinakubalika kama cha kawaida cha kolesteroli mwilini kwa mtu chini ya miaka 30 kilikuwa mg 120 mpaka 290 huku ikikubalika 150 mpaka 340 kwa mtu wa miaka zaidi ya 40.

Kwa mjibu wa viwango vinavyokubalika sasa, ikiwa majibu ya kipimo cha “lipoprotein (protini inapochanganyana na mafuta) profile” yanaangukia katika usawa ufuatao, utachukuliwa kama huna tatizo na hutakiwi kuwa na wasiwasi juu ya hilo:

  • Jumla ya kolesteroli: chini ya 200 mg/dl
  • Msongamano wa juu wa lipoprotini kolesteroli: zaidi ya 40 mg/dl
  • Msongamano wa chini wa lipoprotini kolesteroli: kati ya 100-129 mg/dl
  • Triglycerides: chini ya 150 mg/dl

Umeona tofauti kubwa ya kiasi cha kolesteroli iliyokuwa inakubalika 1970 na ile inayokubalika siku hizi?.  Kwanini kiasi hiki kilipunguzwa?
Ni watu milioni ngapi zaidi wanatumia dawa za kupungunguza/kudhibiti kolesteroli siku hizi kwa sababu kiasi kilichokuwa kinakubalika kilipunguzwa na kwa gharama gani?.

Kwa mjibu wa William Campbell Douglass, M.D., ambaye amekuwa akitibu watu wenye kolesteroli duniani kote kwa zaidi ya miaka arobaini sasa, ikiwa jumla ya kolesteroli yako ni kati ya 200 na 300 na unatumia chakula safi chenye wanga mchache, usijisumbuwe kuwaza kuhusu kolesteroli.

Edward R. Pinckney, M.D. katika kitabu chake “The Cholesterol Controversy” anatuambia kwamba watu waliolazimishwa kupunguza kiasi chao cha kolesteroli kwa sababu wameonekana kuwa na shambulio la moyo walijikuta wakitokewa kupatwa na shambulio jingine la moyo kuliko wale walioendelea kula kawaida bila kuzidisha.

Je kutoa damu kunaweza kusababisha kiasi chako cha kolesteroli kupanda ju?:

Amini usiamini, kwa baadhi ya watu, wazo tu la kutoa damu linaweza pelekea kolesteroli zao kupanda juu mpaka 400 hata kama hawana tatizo na kolesteroli kwa ujumla.

Tuchukulie mfano umefadhaishwa kiasi kidogo tu kwa kupimwa kiasi cha kolesteroli – labda kwa sababu ya kushikiwa tu sindano juu ya mkono wako kunakuudhi au kwa sababu tayari unahofu kupima kiasi cha kolesteroli ulichonacho kinachoelea katika mkondo wako wa damu kunaweza kumaanisha una ugonjwa wa moyo – hivyo majibu ya kiasi cha kolesteroli yatakayopatikana ukiwa katika hali hii yanaweza kuwa si ya kweli kwa karibu ya asilimia 100.

Wakati unaweza kuwa tu na kolesteroli ya kiasi cha 180 mg ambacho kinachukuliwa kuwa ni cha kawaida, hofu, wasiwasi au woga vyaweza pelekea kupanda kwa kiasi cha kolesteroli na majibu ya maabara yanaweza kutoka na 360 mg kiasi kinachotosha kukufanya wewe (pengine hata daktari wako) kuanza mzunguko usioisha (vicious cycle) kutibu ugonjwa wa moyo kwa madawa.

''Tangu mwaka 1936, utafiti baada ya utafiti umeonesha
hakuna uhusiano kati ya kolesteroli na ugonjwa wa moyo.''


Utafiti wa kwanza kuhusu kolesteroli na ujikusanyikaji wake katika ateri (atherosclerosis) umewahi kuchapishwa 1936. majibu ya mwisho yalionesha kuwa hakukuwa na uhusiano kabisa kati ya kiasi cha kolesteroli katika damu na dipositi za kolesteroli katika ateri.

Utafiti mwingine mwaka 1963 ukihusisha askari wastaafu 800 (wa Marekani) juu ya miaka 60, ulionesha kwamba ateri za waliokuwa na kolesteroli chache hazikuwa na tofauti na za wale wenye kolesteroli kuzidi.

Dr. Michael DeBakey mtaalamu maarufu mmarekani katika masuala ya upasuaji wa moyo na timu yake ya utafiti walitafiti waathirika 1700 wenye ateri zilizozibika au kukazika (arteriosclerosis). Nane kati ya kumi ya waathirika hawa walikutwa na kolesteroli ya kawaida inayokubalika kwa wamarekani.

Dr. William P. Catelli, mkurugenzi wa utafiti maarufu wa Framingham study, ambaye ametafiti sababu zote zinazoweza pelekea ateri kuzibika au kukazika na ugonjwa wa moyo, alitamka kwa mara ya kwanza katika historia mwaka 1992 kwamba....

“….ndani ya Framingham, wengi wa watu, kadiri walivyokula mafuta yatokanayo na wanyama (saturated fat) ndivyo walivyopata kolesteroli nyingi, na ndivyo watu hao walipata kuwa na kalori/nishati nyingi, na ndivyo watu hao walivyokutwa na damu chache yenye kolesteroli…”  !!!
Anaendelea...

“Tulipata kujuwa kuwa watu waliokuwa wakila vyakula vyenye kolesteroli nyingi, walikula kolesteroli itokanayo na wanyama (saturated fat), walikutwa na kalori nyingi, uzito wa wastani na walikuwa na miili yenye nguvu (physically active.)”


Hadithi tisa kuhusu kolesteroli:

  • Vyakula vyenye mafuta mengi husababisha ugonjwa wa moyo.
  • Kolesteroli nyingi husababisha ugonjwa wa moyo.
  • Vyakula vyenye mafuta mengi hupandisha kolesteroli kwenye damu.
  • Kolesteroli huziba ateri
  • Utafiti kwa wanyama unathibitisha wazo la lishe kwa ajili ya moyo.
  • Kupunguza kolesteroli yako kunaongeza urefu wa kuishi.
  • Mafuta yatokanayo na mbogamboga (Polyunsaturated) ni bora kwa afya yako.
  • Kampeni dhidi ya kolesteroli imeegemea katika sayansi chanya/ukweli.
  • Wanasayansi wote wanaunga mkono lishe yenye kolesteroli chache ili kulinda moyo.


Hadithi zote tisa hapo juu zimethibitishwa kuwa si za kweli na zimeelezewa kwa kina zaidi katika kitabu: “The Cholesterol Myths” kilichoandikwa na Uffe Ravnskov, MD, PhD. Kitabu kizuri kwa anayependa kujifunza ukweli kuhusu kolesteroli.

Zifuatazo ni baadhi ya kweli:
  • Watu wenye kolesteroli chache hutokewa pia na kuzibika au kukazika kwa ateri (atherosclerotic) kama ilivyo kwa watu wenye kolesteroli kuzidi.
  • Watu wazee wenye kolesteroli nyingi huishi miaka mingi.
  • Kolesteroli nyingi hukukinga dhidi ya magonjwa ya kuambukizana (infectious diseases).

Alipoulizwa ikiwa mafuta yatokanayo na wanyama (saturated fats) husababisha ugonjwa wa moyo, Mary G. Enig, MD PhD, alijibu:  “Wazo kwamba mafuta yatokanayo na wanyama husababisha ugonjwa wa moyo halina ukweli hata kidogo, lakini taarifa hizo zimechapishwa mara nyingi zaidi katika miongo mitatu au zaidi iliyopita kiasi kwamba ni vigumu kuwashawishi watu tofauti labda kama wapo tayari kuchukuwa muda kusoma na kujifunza sababu za kiuchumi na kisiasa zilizotengeneza ajenda dhidi ya mafuta yatokanayo na wanyama (anti-saturated-fat agenda).”




Triglycerides na Trans fats:


Kitu kingine unachohitaji kuwa makini nacho ni triglycerides. Trglcerides (mafuta yapatikanayo katika damu) yanaweza kuchangia kutika kukazika kwa ateri (atherosclerosis) au kuzifanya ateri kuwa na kuta zenye maki kubwa jambo linaloweza pelekea kuongezeka kwa hatari ya kupatwa na shambulio la moyo, ugonjwa wa moyo, mishtuko au kisukari.

Triglycerides ni aina ya mafuta yapatikanayo katika damu yako. Wakati unakula, mwili wako hubadilisha kalori yeyote ambayo haina matumizi nayo muda huo na kuwa triglycerides na kuihifadhi katika seli zako za mafuta. Baadaye, wakati mwili unahitaji diseli ili kutembea, utayatumia mafuta hayo yanayohifadhiwa katika damu (triglycerides) ili kuzarisha nguvu.

Ikiwa unazoea kula chakula kuzidi ya ulivyopaswa na haujishughulishi kutembea kwa miguu au kufanya mazoezi japo kidogo na kukaa tu muda wote ukiangalia televisheni muda wote, inaweza kukutokea kuwa na usawa uliozidi wa triglyceride.

Linapokuja suala la aina za mafuta katika lishe zako, unajitahidi kukwepa mafuta magumu/ya mgando (trans fats) kwa gharama zozote .

mwaka 1958, Ancel Keys, ambaye alisomea magonjwa yahusianayo na moyo, alikuwa mmoja wa watu wa mwanzo kuandika kuwa mafuta yatokanayo na mboga mboga yaliyoongezwa haidrojeni (hydrogenated vegetable oils) na mafuta yake magumu/mazito (trans fatty acids) ndio wahusika wakuu katika kutengeneza ugonjwa wa moyo.

Yanachofanya mafuta haya:
  • Yanashusha msongamano wako wa juu wa lipoprotini (HDL) kolesteroli.
  • Yanapandisha msongamano wako wa chini wa lipoprotini (LDL) Kolesteroli
  • Yanaweza kuupandisha usawa usawa wako wa triglyceride
  • Yanaweza kuharakisha pumu/asthma za utotoni

Badala ya kukupatia afya, trans fats yanakusaidia kukusogeza hatua moja zaidi karibu na kaburi.

Ni mafuta gani hayo? Trans fats (transifatsi) ni mafuta yanayotengenezwa kwa kuchanganya haidrojeni na mafuta yatokanayo na mboga mboga kupitia mbinu iitwayo‘’hydrogenation’’.  Trans fats huwa ni magumu (kama mafuta ya mgando) zaidi ya mafuta mepesi jambo linalosaidia yasiharibike haraka.

Kwahiyo, utakapoenda nje tena kufanya manunuzi ya chakula, tafadhari soma vibandiko vya bidhaa (labels). Ikiwa utasoma kibandiko chenye neno ‘’hydrogenated’’ sehemu yeyote, fikiria mara mbili kabla hujanunua.

Mwishoni mwa miaka ya tisini (1990) tafiti katika mishtuko ya moyo zilionesha watu waliokuwa wanapendelea zaidi mafuta yatokanayo na mboga mboga (polyunsaturated fats) walikuwa na uwezekano zaidi wa kupatwa na mishtuko ya moyo (strokes), na kupungukiwa usawa wa mafuta yatokanayo na wanyama (saturated fats). Iliripotiwa pia kuwa watu wa rika la juu waliokuwa na usawa wa kolesteroli chini ya mg 200 katika damu walikuwa na hatari kubwa zaidi ya kupatwa na mishtuko ya moyo.

Ikiwa una mojawapo ya hali hatarishi zifuatazo, unaweza kuwa kandideti wa kolesteroli kuzidi:
  • Lishe duni: kutumia vyakula pekee vyenye mafuta ya mboga mboga, kutumia mafuta yaliyochanganywa na haidrojeni na kutumia trans fats
  • Usawa uliozidi wa triglyceride mwilini
  • Ukosefu wa mazoezi: Mazoezi husaidia kuuongeza msongamano wako wa juu wa lipoprotini (kolesteroli nzuri) huku yakishusha msongamano wako wa chini wa lipoprotini (kolesteroli mbaya)..
  • Shinikizo la juu la damu: kuongezeka kwa presha katika kuta zako za ateri huharibu ateri zako jambo linaloweza kuongeza spidi ujikusanyikaji wa dipositi za mafuta

Kolesteroli huokoa maisha yetu: 

Nini ungefanya ikikutokea umeanguka na kujichubua goti vibaya? Kwanza utaliosha goti vizuri kwa maji kisha utapaka mafuta kidogo na kufunika na bandeji. Baada ya siku kadhaa, utaitoa bandeji na goti litaonekana kama halijawahi kupatwa na mchubuko wowote.  Ndiyo, mwili wako unao uwezo wa kutenda kama wewe ulivyotenda na bandeji.

Dr. Batmanghelidj anasema damu yenye asidi inayotokea mapafuni inaweza kuelea mpaka kwenye moyo. Wakati damu hii yenye asidi inapoondoka katika moyo wako huanza kuvuta maji nje ya seli zinazozunguka ateri zako na kusababisha michubuko midogo midogo (microscopic abrasions) na machozi.

Hii michubuko midogo midogo na machozi katika ateri ni kama mchubuko ulioupata ulipojikwaa na kuanguka kama tulivyoona hapo juu. Mwili wako sasa utatumia hayo ‘’mafuta’’ kama bandeji isiyopitika maji (water proof bandage) yaani Kolesteroli ili kuzifunika seli zinazozunguka ateri.
Kwa watu wenye afya zao, miili yao sasa itaiita kinga ya mwili kwenda katika ‘’bandeji’’ hiyo (kolesteroli) na kuanza kuliripea tatizo na mwishowe kuiondoa bandeji ya kolesteroli.
Ndiyo, mwili wako unao uwezo wa kujiripea wenyewe. Isitoshe mchubuko ule kwenye goti lako ulipona, au siyo?.

Ni kweli, kama hautabadili tabia katika lishe na staili za maisha yako, mwili kamwe hautapata nafasi ya kujiripea wenyewe. Kolesteroli zaidi na zaidi itatupwa juu ya hii michubuko na pengine kukupatia mapigo au shambulio la moyo katika siku za baadaye.

Kama miili yetu haitengenezi kolesteroli kufunika michubuko ambayo hujitokeza katika ateri kwa baadhi yetu, hatimaye michubuko hiyo midogo midogo (microscopic abrasions) huendelea kuwa mikubwa na yenye kina kiasi cha ateri kuachana wazi na kusababisha kifo cha ghafla.

Dr Batmanghelidj anasema katika vitabu vyake nilivyosoma: “kama tunaupatia mwili maji yake ya mhimu kabla ya kula chakula, mapigano yote dhidi ya uundwaji wa kolesteroli katika mishipa ya damu yatakuwa yameonywa.”

Kwanini?….kwa sababu kwa kunywa maji halisi pamoja na kiasi kidogo cha chumvi nusu saa kabla ya chakula, seli ndani ya mwili zitakuwa zimefanikiwa kujazwa maji (hydrated). Mwili wako hautahitaji kuvuta maji toka katika ateri zako kusaidia kumeng’enya chakula.
Fanya hivi kila siku na damu yako haitakuwa ikijikusanya tena (concentrate), kwahiyo haitaendelea kuvuta maji toka katika seli kuzunguka kuta za ateri jambo litakalokomesha kujitokeza kwa michubuko midogo midogo.
Zoezi hili (la kunywa maji kabla ya kula) litazuia dipositi za kolesteroli kujikusanya katika ateri zako. Hatimaye, baada ya muda, dipositi hizi za kolesteroli zitapotea labda kama zitakuwa zimeshaunguzwa (calcified).

Mazoezi, Mazoezi, Mazoezi:

Wakati mmoja Dr. Batman alikutana na bwana mmoja mwenye rika la miaka arobaini hivi akisumbuliwa na kuzibika kiasi ateri zake ziendazo katika moyo, jambo lililokuwa likimsababishia maumivu ya kifua.
Bwana huyo alikuwa afanyiwe upasuwaji, lakini Dr Batman akamshauri kujaribu tiba mubadala kabla ya kujaribu kujiingiza katika upasuwaji kuona kama ingemsaidia. Bwana huyo alikubali na akanza kurekebisha unywaji wake wa maji na utumiaji wa chumvi na akaanza kunywa maji kila nusu saa kabla ya kila mlo. Pia akaanza kutembea kwa miguu dakika ishirini mpaka therathini asubuhi na jioni (akiongeza dakika kidogo kidogo mpaka lisaa limoja). .

Miezi mitatu baadaye, mtu huyo akaenda kufanya vipimo vyake vya mwisho kuona kama bado anahitaji kuhamia kufanya upasuwaji. Vipimo vya maumivu kifuani (angiogram test) havikuonesha ishara yeyote ya kuzibika kwa ateri. Hakuwa anahitaji tena upasuwaji.

Tunazaliwa na miguu ili kutembea. Mazoezi ni kutembea na kutembea ni afya bora. Ikiwa unaweza kutembea tu dakika tano, anzia hapo. Unatakiwa tu kuongeza tu dakika tano kila siku asubuhi na jioni mpaka utakapoweza kutembea lisaa lizima kwa pamoja asubuhi na jioni. Kutembea ni jambo jema kwa mifupa yako, mzunguko wa damu, kolesteroli na kudhibiti mafuta kuzidi.


Swali: Ni sehemu gani mwilini ambako sehemu kubwa ya kuzibika kwa ateri sababu ya kolesteroli hutokea?.

Jibu: Katika ateri karibu na moyo wako na katika ateri zilizopo shingoni mwako.

Tumeambiwa kuwa ni ‘’usawa wa kolesteroli’’ katika damu zetu ambao husababisha dipositi za kolesteroli ndiyo husababisha mapigo na shambulio la moyo.

Swali: Unapofanyiwa vipimo vya usawa wa kolesteroli, kwa kawaida sampuli ya damu hutolewa toka kwenye veini katika mkono wako.
Ikiwa ni kweli ni ‘’usawa wa kolesteroli’’ katika damu yako ndiyo unaoweza kusema iwapo upo katika hatari ya kuwa na ugonjwa wa moyo, kwanini sasa hakujawahi kuwa na rekodi ya kuzibika kwa veini au kapilari?... Kwa sababu damu huelea kupitia ‘’veini na kapilari’’ hizi ndogo taratibu zaidi kuliko katika ateri, siyo tulipaswa kupata kuzibika kwa veini na kapilari kabla hatujapatwa na kuzibika kwa ateri?.

Jibu: Muulize Daktari wako…….lakini ikiwa tu unahitaji kukodolewa naye macho!


Mwanga wa jua husaidia kushusha usawa wa kolestroli:

Je wajuwa kuwa mwanga wa jua huibadilisha kolesteroli iliyomo kwenye damu yako na kuwa vitamini D?.
Maana yake ni kuwa unaweza kuipunguza kolesteroli yako kwa kutembea nje katika mwanga wa jua. Kwanza, unahitaji kuuweka mwili wako zaidi kadili iwezekanavyo moja kwa moja katika miale ya jua. Usipake chochote juu ya ngozi (sunscreen) kuzuia ukali wa mwanga wa jua, kwani nyingi ya hizo zimetajwa kuwa na kemikali zinazosadikika kusababisha kansa na zinazuia miale yote ya jua kuingia mwilini.

Kiasi gani hasa cha jua?:

Jua la kutosha kuweza kufanya ngozi yako kuwa ya uwaridi hivi. Unapofikia hali hii ya uwaridi, mwili wako hautaweza kuendelea kutengeneza vitamini D. Ukiendelea kubaki juani baada ya ngozi kufikia hali hii utakuwa unaenda kuleta madhara tu katika ngozi yako.
Mimi kwa kawaida hutoa kabisa shati na kubaki nakaptula na ndipo naanza kuzunguka juani mpaka nichoke (huwa porini lakini).

Kwa hakika kabisa unaweza kuzarisha mpaka uniti 20,000 za vitamini D kwa siku kupitia staili hii ya kujianika juani. Hata hivyo, hauhitaji kujishughurisha sana na kiasi gani cha vitamini D unatengeneza kwani ngozi yako inayo majibu ambayo yatafunga uzarishaji wa vitamini D ukifikia hatua ya uwaridi.
Kadili unavyopata usawa mahususi wa kolesteroli katika mwili wako utakuwa pia ukitengeneza vitamini D chache kwa kawaida, kwa hiyo hakutakuwa kamwe na hatari ya kuzidisha dozi ya kupata vitamini D yako toka katika jua.

Mstari mmoja wa habari, kukaa nyuma ya dirisha au kupaka chochote kuzuia mwanga wa jua usikukute moja kwa moja katika ngozi yako, vitaizuia miale ya jua (ultraviolet-B) kuweza kugonga juu ya ngozi yako na hivyo kushindikana kwa kolesteroli kuwa vitamini D.

2 comments:

Twitter Bird Gadget