Friday, April 20, 2012

Tafsiri sahihi ya 'sala ya BWANA'


WAKRISTO wote duniani kila siku wanasoma sala (dua) waliyofundishwa na Mtume Yesu (a.s.). Sala hii kwa kuwa ndio msingi mkubwa wa ibada ya Kikristo, wameitukuza sana na kuiita "sala ya Bwana" au "Baba yetu". Lakini ni kweli Wakristo wanajua tafsiri sahihi ya maneno hayo? Au yanatoka mdomoni tu bila kujua wanasema nini. Mimi nadhani endapo wangejua maana ya dua hiyo ya Mtume Yesu (a.s.), Marais, wafalme, mawaziri wakuu na viongozi wengine wa Kikristo wasingekanyaga Makanisani wala kuthubutu kutamka maneno hayo matakatifu sana. InshaAllah katika makala hii nitafasiri dua hiyo ili kujua ni kitu gani kilikusudiwa na Mtume Yesu (a.s.). Kabla ya kufasiri maneno hayo, kwanza tuzingatie kuwa, maneno hayo hayakusemwa na mlalahoi kama mimi. Bali yamesemwa na Mtu mtakatifu na mtukufu sana. Yesu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kama anavyojishuhudia mwenyewe (Yohana 17:3). Hivyo lolote analosema ametumwa na Mwenyezi Mungu (Yohana 14:1-11). Kwa hiyo "sala ya Bwana" sio maneno ya Yesu (a.s.) binafsi bali ni aya (maneno) ya Mwenyezi Mungu. Hivyo lazima tuyape uzito wa hali ya juu sana.
Hapa nitanukuu dua yote, kisha nitafasiri aya moja moja. " Bali ninyi salini (ombeni) hivi; "9. Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, ufalme wako uje, 10. Mapenzi yako yako yatimizwe, hapa duniani kama (huko) mbinguni. 11. Utupe leo riziki yetu. 12. Utusamehe deni (makosa) zetu, kama sisi nasi tuwasamehavyo wadeni (waliotukusoea) wetu. 13. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe (utukinge) na yule mwovu (shetani) kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina". (Mithayo 6:9-13)
Tafsiri:
Aya ya 9: Yaani, wanadamu sote, Baba yetu halisi wa kiroho na kimwili yuko mbinguni ambaye ni Mwenyezi Mungu (s.w.). Hivyo jina lake litukuzwe kuliko mtu yeyote, kitu au hali yoyote ile. Maneno haya yamerejewa katika agano jipya (Qur'an) linasema "Basi litukuze jina ma Mola wkao aliye mtukufu". (87:1). Ili kutimiza agizo hili, Waislamu tunasema tasbihi hizi katika kila rkuu na sujud zetu. Aya hii ya tisa ilimalizia na maneno "ufalme wako uje". Maneno haya yanadhihirisha kuwa, wakati anafundisha dua hii, bado ufalme wa Mwenyezi Mungu haujaja (haupo).
Hivyo anawahimiza wafuasi wake wamuombe Mwenyezi Mungu awaondolee utawala wa shetani uliopo na kuwawekea ufalme wa Mweneyzi Mungu. Aidha aliwahimiza wafanye jitihada (jihad) ya hali ya juu ili kufanya mapinduzi hayo. Anasema "Msisumbuke, basi mkisema, tule nini? au tunywe nini? au tuvae nini? kwa maana hayo yote mataifa (makafiri) huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni (upiganieni) kwanza ufalme wake, na haki yake, na hayo yote mtazidishiwa" (Mathayo 6:31-33)
Aya ya 10: "Mapenzi (matakwa) yako yatimizwe...". Kwanza tujue matakwa ya Mwenyezi Mungu yanatimizwa vipi huko mbinguni. Sote tunajua kuwa, baada ya ibilisi kufukuzwa, hakuna kiumbe chochote kilichobaki huko kinachomwasi Mwenyezi Mungu. Ibilisi alipotumwa duniani, alipewa madaraka ya kutawala dunia (Taz. Yohana 12:31, Yohana 16:11 n.k.). 
Hivyo anataka makhalifa wake (marais, wafalme, mawaziri wakuu, masultani n.k.) na kuwapangia sehemu (nchi) watakayotawala kwa niaba yake. Kwa sababu hiyo Mtume Yesu (a.s.) anawahimiza wafuasi wake wamwombe Mwenyezi Mungu awaondolee utawala wa shetani na makhalifa wake, ili kisiwepo "kinyago" chochote kiwe Rais, Mfalme, Sultani, Waziri Mkuu n.k. kitakachong'ang'ania madaraka (ufalme) kinyume na mapenzi (matakwa) ya Mwenyezi Mungu (s.w.).
Aya ya 11: Utupe leo riziki yetu". Yaani riziki (neema) zote (uzima, nguvu, hewa, chakula, maji n.k.) hakuna azitoaye ila Mwenyezi Mungu peke yake. Hivyo tusimtegemee kiumbe yeyote atupe chakula, ulinzi, uzima, nguvu au chochote kile kinyume na atoavyo Mwenyezi Mungu.
Aya ya 12: "Utusamehe makosa yetu..." Yaani makosa yote na madhanmbi yote makubwa na madogo, hakuna tunayemkosea ila Mwenyezi Mungu. Kwani viumbe vyote vilivyoko duniani ni vyake. Hivyo kuua, kudhuru, kudhulumu au kusumbua kiumbe chochote (binadamu, mnyama, ndege, mdudu n.k.) bila idhini ya Mwenyezi Mungu ni madhambi makubwa. Aidha viungo vya mwili na neema zote tumepewa na Mwenyezi Mungu ili zitusaidie katika lengo la kuumbwa la kumtii Mwenyezi Mungu (s.w.). Hivyo kutumia kiungo chochote cha mwili au neema yoyote (madaraka, kazi, nguvu, n.k.) kinyume na Mwenyezi Mungu ni kumkosea Mwenyezi Mungu kwa kiwango cha juu sana. Kwa kuwa hakuna tunayemkosea isipokuwa Mwenyezi Mungu, vile vile hakuna anayesamehe isipokuwa Yeye peke yake. Hivyo tumuombe msamaha na tukome kuendelea kufanya maasi hayo makubwa.
Aya ya 13: "Usitutie majaribuni..." Yaani tumuombe Mwenyezi Mungu (s.w.) atuondolee mambo yote yanayotushawishi kumuasi Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema "Naye atasema, Tutieni, tutieni (katika sheria ya Mwenyezi Mungu), itengenezeni njia, kiondoeni kila kikwazo katika njia ya watu wangu". (Isaya 57:14). 
Baadhi ya ya vishawishi vianvyomiwa na shetani kuwakwaza watu hivi sasa ni pombe na viwanda vyake, kondom na viwanda vyake, mabaa, makasino, mahoteli yanayoitwa "ya kitalii", sinema na video za kipuuzi, madansi, madisko, michezo inayowaghafilisha na ibada (sala, funga n.k.), mikusanyiko inayowachanganya wanawake na wanaume bila dharura, sheria, kanuni au utaratibu unaohamasisha watu kufanya maasi, vifaa na matangazo yanayohmiza ufisadi pamoja na viongozi, wahimizaji na washiriki wa vishawishi hivyo. Hivyo Mtume wetu mtukufu Yesu (a.s.) anatufundisha tumwombe Mwenyezi Mungu atuondolee uchafu huo na mwingine.
Dua (sala) inamalizia kwa maneno "Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu na utukufu, hata milele. Amina". Yaani ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu peke yake. Hivyo falme (dola) zote duniani lazima zifuate utaratibu alioupanga. Yaani Uislamu (unyenyekevu kwa sheria za Mwenyezi Mungu) na kufuata katiba zake zikiwa Torati zamani (agano la kale) na hivi sasa Qur'an (agano jipya). Hivyo falme zote zinakwenda kinyume na katiba ya Mwenyezi Mungu, ni jambo lililoko chini ya mfalme Ibilisi. 
Hivyo lazima jimbo hilo liangamizwe. Aidha nguvu na utukufu ni vyake peke yake.
Hivyo kisiwepo "kinyago" (mtawala) kikajipa nguvu (jeshi, polisi, usalama wa taifa n.k) na kujitukuza kwa kujiita "mtukufu" kinyume na Mwenyezi Mungu (s.w.). Mtume Yesu (a.s.) anasisitiza kwa kuomba kuwa, hali hiyo ya kutukuzwa Mwenyezi Mungu iwe tangu kusimama kwa ufalme wake hapa duniani hadi mwisho wa dunia ("... hata milele"). Dua inaishia na neno "Amina". Yaani na iwe hivyo. Yaani Mwenyezi Mungu atutekelezee tuliyoomba yote kuanzia mwanzo wa dua hadi mwisho wake.
Lakini kabla sijaendelea, naona niweke wazi kuwa, dua niliyoifasiri ni maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.) kupitia Mtume wake Yesu (a.s.). Hivyo sio dua ya "Kikristo", bali ni dua kwa wanyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu (Waislamu). Kwa hiyo Muislamu asiogope kuomba dua hiyo kwa kudhani eti ni sala ya "Kikristo". Tukumbuke kuwa Mtume Yesu (a.s.) hakuwa Mkristo bali Muislamu (mtiifu kwa Mwenyezi Mungu).
Sasa naendelea, Mtume Yesu (a.s.) akituhakikishia kujibiwa kwa dua hiyo anasema; "Nani nawaambia, ombeni, nanyi mtapewa, tafuteni, nanyi mtaona, bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa kuwa kila aombaye hupokea, naye atafutaye (ufalme wa Mungu n.k.) huona; naye abishaye atafunguliwa. Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanaye akimwomba mkate, atampa jiwe? Au samaki; badala ya samaki atampa nyoka? Au akimwomba yai, atampa nge? Basi ikiwa ninyi ndio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, Je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu (nguvu takatifu) hao wamwombao?" (Luka 11:9-13).
Akasisitiza zaidi anasema; "Tena siku ile (mtakayoomba) hamtaniuliza neno lolote atawapa kwa jina (utukufu - yaani kuomba kama alivyofundisha) langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu (yaani kama alivyofundisha); ombeni, nanyi mtapata, furaha yenu iwe timilifu". (Yohana 16:23-24).
Ilibidi Mtume Yesu 9a.s.) atufundishe sisi wafuasi wake dua hiyo kwani Mwenyezi Mungu (s.w.) anasema; "Kwa maana BWANA ndiye mwamuzi (hakimu) wetu; BWANA ndiye mfanya sheria wetu; BWANA ndiye mfalme wetu, ndiye atakayetuokoa". (Isaya 33:22).
Hivyo ametuhimiza tuombe dua hiyo ili Mwenyezi Mungu atupe uwezo na nguvu takatifu (roho mtakatifu) ili tuowaondoe waamuzi (majaji, mahakimu n.k.) wasiohukumu kwa sheria za Mwenyezi Mungu, tuwaondoe "Waheshimiwa" wanaogombania kondom waliojipa kazi ya Mwenyezi Mungu ya kutunga sheria na tuwaondoe na kuwafuta kabisa Marais, wafalme, mawaziri wakuu n.k. waliomnyang'anya Mwenyezi Mungu Uungu na ufalme na kujipa wao ili wafanye ufisadi katika dunia ya Mwenyezi Mungu.
Labda swali hapa ni kuwa "inakuwaje Rais, Mfalme, Waziri Mkuu, Mbunge n.k aende Kanisani kujiombea dua hiyo (Baba yetu) ya hatari kwake? Mwenyezi Mungu anatujibu; "Nitawaepusha na (kuzingatia) aya zangu wale wanaotakabari katika nchi pasipo haki, na ambao kila hoja wanayoiona hawaiamini; na kama wakiiona njia ya uwongofu hawaishiki kuwa ndio njia; lakini wakiiona njia ya upotofu (upotevu) wanaishika kuwa ndio njia. Hayo ni kwa sababu ya kukadhibisha aya zetu na kuzipuuza". (Qur. 7:146) (Angalia pia Mathayo 13:10-15). Hapo tunathibitishiwa kuwa, mtu yeyote dhalimu au Muislamu aliyeshiba unafiki sawa sawa, hawezi kuelewa maonyo yoyote yale mpaka achinjwe.
Kanuni ya kujenga upya siku zote ni kuvunja kabisa jengo (mfumo) la zamani, kisha kujenga upya kabisa. Mwenyezi Mungu anasema; "Angalia nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza, ili kujenga na kupanda". (Yeremia 1:10).
Operesheni hii ya Mtume Yesu (a.s.) ni rahisi sana tukitumia silaha zifuatazo; Kwanza, Ucha Mungu wa hali ya juu sana, pili, kumtegemea moja kwa moja Mwenyezi Mungu peke yake, tatu, kutumia kwa mwisho wa uwezo wetu neema zote tulizopewa na Mwenyezi Mungu (akili, nguvu, mali, madaraka, kazi, silaha n.k.). 
Mwenyezi Mungu ameshasema; "... Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo katika nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu anapowatakia watu adhabu hakuna cha kuzuia wala hawana mlinzi yeyote badala yake". (Qur. 13:11).
Silaha muhimu ya mwisho ni kusubiri na kuvumilia sana kwa lolote litakalotupata. Kwani halitatupata ila lile tu alilokadiria Mwenyezi Mungu (s.w.). Cha kukumbuka sana ni kuwa, sisi ni waja wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea kupitia risasi, ugonjwa, ajali au njia yoyote ile aliyotupangia.
Aidha tukumbuke kuwa mkuu wa operesheni hii (Mtume Yesu a.s.) ameshasema yafuatayo; " Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; La! Sikuja kuleta amani, bali Upanga". (Mathayo 10:34). 
Hivyo hatuna chochote tutakachotumia kufanya kazi yake (kusimamisha ufalme wa Mwenyezi Mungu) zaidi ya hicho alichotuletea kitumike (upanga - AK-47). Mwenyezi Mungu ameshatuwekea kanuni (Law sio theory walaprinciple) kuwa hakuna amani kwa wanaomuasi.
Anasema; "Mimi nayaumba matunda ya midomo (yaani matukio yanayoagizwa na midomo ya watu); amani, amani kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA, nami nitamponya. Bali wabaya wanafanana na bahari iliyochafuka, maana haiwezi kutulia, na maji yake hutoa tope na takataka. Hapana amani kwa wabaya asema Mungu wangu". (Isaya 57:19-21).
Mwisho nawakumbusha Wakristo na Waislamu wenzangu kuwa, sisi sote tunategemea Mtume Yesu (a.s.) atarudi wakati wowote kabla ya mwisho wa dunia. Na sote tunakubaliana kuwa yeye ni mtu mtakatifu sana, hadi Wakristo wakavuka mpaka na kumwita ni "Mungu" au "Mungu Mwana". Pamoja na tofauti za tafsiri zetu, lakini sote tunakubaliana kuwa, Yesu ni mtakatifu sana, hivyo hataridhia atakapokuja aone uchafu na dhulma iliyojaa duniani. Na ikizingatiwa kuwa tayari alishatoa agizo la kuondoa ufalme wa shetani na makhalifa wake, atakasirika sana akikuta bado hatujatekeleza agizo lake.
Atakasirika zaidi akigundua kuwa japo baadhi ya waliomwamini wamemtukuza sana hadi kumuita 'Mungu' au 'Mungu Mwana', lakini watu hao hawataki kutekeleza agizo lake alilolitoa zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita. Hivyo ni wajibu wetu sisi tuliomwamini (Waislamu na Wakristo) tushirikiane kwa hali na mali kutekeleza operesheni hii tuliyoagizwa, ili mwenyewe atakapokuja akute tayari kazi tumeimaliza au tumeuawa kwa ajiil yake. Asema "Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili wala mtu apendaye mwana au binti kuliko mimi hanistahili. Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili, mwenye kuiona (kuikinga) nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza (kujitoa muhanga) nafsi yaek kwa ajili yangu ataiona". (Mathayo 10:37-39)
Namalizia kwa maneno matakatifu yafuatayo: "Lakini yeye anayenitumaini ataimiliki nchi, na kuurithi mlima wangu mtakatifu". (Isaya 57:13).
"Maana watenda mabaya wataharibwa, bali wamgnojao BWANA ndio watakaoirithi (watakaoitawala) nchi. Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwepo, utapangaalia mahali pake wala hatakuwepo. Bali wenye upole watairithi nchi, watajifurahisha kwa wingi wa amani. Asiye haki hunuia mabaya juu ya mwenye haki, na kumsagia meno yake. BWANA atamcheka, maana ameona kwamba siku yake inakuja. Wasio haki wamefuta upanga na kupinda uta, wamwangushe chini maskini mhitaji na kuwaua wenye mwenendo mnyofu. 
Upanga wao utaingia mioyoni mwao wenyewe. Na nyuta zao zitavunjika. Kidogo alicho nacho mwenye haki ni bora kuliko wingi wa mali wa wasio haki wengi. Maana mikono ya wasio haki itavunjika, bali BWANA huwategemeza wenye haki. BWANA anazijua siku za wakamilifu, na urithi wao utakuwa wa milele. Hawataaibika wakati wa ubaya, Na siku za njaa watashiba (yaani watakapohitaji nusra ya Mwenyezi Mungu watapewa). Bali wasio haki watapotea, Nao wamchukiao BWANA watatoweka, kama uzuri wa mashamba, kama msohi watatoweka. 
Asiye haki hukopa wala halipi (yaani hutoa viapo vya kumtii Mwenyezi Mungu akipewa madaraka, kisha humwasi Mwenyezi Mungu akiwa madarakani au kazini), Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu. Maana waliobarikiwa na Yeye watairithi nchi, Nao waliolaaniwa na Yeye wataharibikiwa". (Zaburi 37:9-22)
"Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na kufanya vitendo vizuri, kuwa atawafanya Makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya Makhalifa wale waliokuweko kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia dini yao aliyowapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao, wawe wananiabudu, hawanishirikishi na chochote. Na watakaokufuru baada ya hayo; basi hao ndio wavunja amri zetu". (Qur. 24:55).

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget