Uislamu umejengwa katika nguzo tano za Kiislamu na nguzo ya pili ni Sala, na kuacha kusali ni moja ya dhambi katika madhambi makubwa sabini. Mtume S.A.W. kasema katika Hadithi iliyopokelewa na Ibn Umar R.A.A. na kutolewa na L-Bukhari na Muslim, “ ‘‘بُنِيَ الإسْلامُ عَلَى خَمْسٍ : شَهَادَةِ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ وَإِقَامِ الصَّلاةِ وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ وَصَوْمِ رَمَضَانَ وَحَجِّ الْبَيْتِ’’Maana yake, “Umejengwa Uislamu kwa nguzo tano, (nguzo ya kwanza): Hapana mungu mwenye kupasa kuabudiwa ila Allah, na hakika Muhammad S.A.W. ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na (nguzo ya pili): Kusimamisha Sala, na (nguzo ya tatu): Kutoa Zaka, na (nguzo ya nne): Kufunga (mwezi wa) Ramadhani na (nguzo ya tano): Kuhiji (nyumba ya Mwenyezi Mungu kwa yule mwenye uwezo).”
Uislamu umehimiza sana Sala kwa sababu ni funguo ya Pepo, na ni amali ya kheri na pia ni uhusiano kati ya mja na Mola wake. Na zile Sala zinamsaidia Mwislamu kumliwaza na juu ya taabu na shida za maisha ya dunia. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Suratil Baqarah aya ya 45, “ وَاسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلاةِ…Maana yake, “Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kusali…”
Kwa jinsi Sala zilivyokuwa muhimu ndio maana Mwenyezi Mungu Mtukufu katuhimiza sana ndani ya Qurani Tukufu tuzihifadhi Sala zote kwa kuzisali kila siku mara tano mchana na usiku kwa wakati wake. Kasema katika Suratil Baqarah aya ya 238, “حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلاَةِ الْوُسْطَى وَقُومُوا لِلَّهِ قَانِتِينَMaana yake, “Zilindeni sana Sala (zote kuzisali, khasa jamaa) na khasa Sala ya katikati, na simameni kwa unyenyekevu katika kumwabudu Mwenyezi Mungu.”
Na Mtume S.A.W. ametuelezea katika Hadithi kwamba tofauti kati ya mja Mwislamu na ukafiri na ushirikina ni KUACHA KUSALI. Kasema katika Hadithi iliyopokelewa na Jaabir bin Abdallah R.A.A. na kutolewa na Ttirmidhi na Muslim, “‘‘بَيْنَ الْعَبْدِ وَبَيْنَ الْكُفْرِ تَرْكُ الصَّلاةِ’’Maana yake, “Tofauti kati ya mja (Mwislamu) na ukafiri ni kuacha Sala.” Na katika Hadithi iliyopokelewa na Buraida R.A.A. na iliyotolewa na Ahmad, Ibn Maajah, Abu Daud, Nnasaai na Ttirmidhi, Mtume S.A.W. kasema, “ ‘‘الْعَهْدُ الَّذِي بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمُ الصَّلاةُ فَمَنْ تَرَكَهَا فَقَدْ كَفَرَ’’Maana yake, “Ahadi baina yetu (Waislamu) na baina yao (makafiri) ni Sala; na atakaeiacha basi kakufuru.”
Na kitendo chochote cha mtu yule asiesali hakikubaliwi na Mwenyezi Mungu S.W.T., wala dua yake haipandi mbinguni ikiwa ni pamoja na adhabu KUBWA SANA inayomngoja kesho Akhera. Mwenyezi Mungu S.W.T kawaonya kwa maonyo makali ya adhabu siku ya Kiyama kwa wale ambao wanapuuzia hawasali, kasema katika Surat Maryam aya ya 59 na ya 60, “فَخَلَفَ مِنْ بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا * إِلاَّ مَنْ تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَأُوْلَئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلا يُظْلَمُونَ شَيْئًاMaana yake, “Lakini wakaandamia baada yao chipukizi mbaya (watoto wabaya). WAKAPUUZIA Sala na wakafuata matamanio mabaya; kwa hivyo watakutana na ADHABU KALI. Isipokuwa wakitubu na kudumu kuamini na kufanya yaliyomema. Hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa chochote.”
Ibn Abbaas R.A.A. kafasiri, “KUPUUZIA” katika aya hii haimaanishi kwamba wameaacha kusali kabisa, lakini wao wana zichelewesha Sala zao mpaka muda wake wa mwisho kabisa.” Na kuchelewesha Sala ni kama ifuatavyo:a) Kuichelewesha Sala ya Adhuhuri mpaka Sala ya Alasiri.b) Kuichelewesha Sala ya Alasiri mpaka Sala ya Magharibi.c) Kuichelewesha Sala ya Magharibi mpaka Sala ya Isha.d) Kuichelewesha Sala ya Isha mpaka Sala ya Alfajiri.e) Kuichelewesha Sala ya Alfajiri mpaka linapoanza kuchomoza jua.
Lakini Mwislamu anatakiwa afuate nyakati sahihi kama ilivyokuja katika Hadithi iliyopokelewa na Abdallah bim `Umar R.A.A. na iliyotolewa na Muslim kasema, “‘‘إِذَا صَلَّيْتُمُ الْفَجْرَ فَإِنَّهُ وَقْتٌ إِلَى أَنْ يَطْلُعَ قَرْنُ الشَّمْسِ الأَوَّلُ ، ثُمَّ إِذَا صَلَّيْتُمُ الظُّهْرَ فَإِنَّهُ وَقْتٌ إِلَى أَنْ يَحْضُرَ الْعَصْرُ ، فَإِذَا صَلَّيْتُمُ الْعَصْرَ فَإِنَّهُ وَقْتٌ إِلَى أَنْ تَصْفَرَّ الشَّمْسُ ، فَإِذَا صَلَّيْتُمُ الْمَغْرِبَ فَإِنَّهُ وَقْتٌ إِلَى أَنْ يَسْقُطَ الشَّفَقُ ، فَإِذَا صَلَّيْتُمُ الْعِشَاءَ فَإِنَّهُ وَقْتٌ إِلَى نِصْفِ اللَّيْلِ’’Maana yake, “Mtakaposali Sala ya Alfajiri wakati wake (wa mwisho) ni mpaka linapoanza kuchomoza jua. Mtakaposali Sala ya Adhuhuri wakati wake (wa mwisho) ni mpaka inapohudhuria Alasiri. Mtakaposali Sala ya Alasiri wakati wake (wa mwisho) ni mpaka jua linapokuwa manjano. Mtakaposali Sala ya Magharibi wakati wake (wa mwisho) ni mpaka inapopotea wekundu. Mtakaposali Sala ya Ishaa wakati wake (wa mwisho) ni mpaka nusu ya usiku.”
Na mtu yeyote yule atakaekufa bila kutubu, yaani kaendelea na hali hiyo hiyo mpaka kufa kwake, Mwenyezi Mungu S.W.T. amemtayarishia GHAY siku ya Kiyama ili iwe ndiyo adhabu yake inayomgoja, nayo ina maana ya wadi katika Jahannamu iliyoko chini kabisa. Na Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Maa`uun aya ya 4 na ya 5, “ فَوَيْلٌ لِلْمُصَلِّينَ * الَّذِينَ هُمْ عَنْ صَلاتِهِمْ سَاهُونَMaana yake, “Basi adhabu itawathubutikia wanaosali. Ambao wanapuuza (maamrisho ya) Sala zao.” Na Hadithi iliyopokelewa na Sa`ad bin Abi Waqqaas R.A.A. na iliyotolewa na Bazaar, “Alimuuliza Mtume S.A.W. kuhusu maana ya “KUPUUZA” na Mtume S.A.W. akajibu akasema, “ ‘‘هو تأخير الوقت’’Maana yake, “Hiyo ni kuchelewesha wakati (wa Sala).”
Mwenyezi Mungu S.W.T. amewaita watu hao “WANAOSALI” wavivu na wanachelewasha Sala zao yaani hawasali kwa wakati wake. Amewaahidi kwa WAYL kuonesha maana ya ADHABU KUBWA. Wanavyuoni wengine wanasema WAYL maana nyingine ni wadi katika Jahannam, wenye moto mkali kabisa. Na hiyo WAYL ndipo patakapokuwa mahali pa wale watu wanaochelewesha Sala zao au leo wanasali na kesho hawasali, ila wale watu watakaotubia na kujirekebisha tabia zao. Jee! Ikiwa huyu anaechelewesha Sala adhabu yake ni KUBWA KABISA basi nini adhabu ya mtu yule asiesali kabisa? Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Munaafiquun aya ya 9, “يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لا تُلْهِكُمْ أَمْوَالُكُمْ وَلا أَوْلادُكُمْ عَنْ ذِكْرِ اللَّهِ وَمَنْ يَفْعَلْ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الْخَاسِرُونَMaana yake, “Enyi mlioamini! Yasikusahaulisheni mali yenu wala watoto wenu kumkumbuka Mwenyezi Mungu; na wafanyao hayo, hao ndio wenye kukhasirika.”
Wafasiri wa Qur-ani wamesema, “Kumkumbuka Mwenyezi Mungu” katika aya hiyo iliyopo hapo juu maana yake, “Kusali Sala tano kila siku.” Na yeyote yule anaeshughulika kwa ajili ya kununua na kuuza, au kwa ajili ya kazi ya kujipatia maisha, au kwa ajili ya watoto wake akasahau Sala atakuwa miongoni mwa waliokhasirika. Mtume S.A.W. kasema katika Hadithi iliyopokelewa na Abu Huraira R.A.A. na kutolewa na Ttirmidhi, “‘‘إِنَّ أَوَّلَ مَا يُحَاسَبُ بِهِ الْعَبْدُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ من عمله صَلاتُهُ ، فَإِنْ صلحت فقد أفلح وأنجح ، وإن فسدت فقد خاب وخسر’’Maana yake, “Kitu cha kwanza atakachohisabiwa mja siku ya Kiyama katika amali yake ni Sala yake. Ikiwa imetengemaa, kafaulu (mtihani) na kanusurika, na ikiwa imeharibika, atakuwa hakufaulu (mtihani) na kakhasirika.”
Pia watu wa Motoni wataulizwa nini sababu ya kuuingia Moto? Kama ilivyokuja katika Suratil Muddathir aya ya 42 na ya 43, “مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ * قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ… Maana yake, “Ni kipi kilichokupelekeni Motoni?” Waseme, “Hatukuwa miongoni mwa waliokuwa wakisali…” Vilevile katika Hadithi iliyopokelewa na Ibn Umar R.A.A. na iliyotolewa na L-Bukhari na Muslim, Mtume S.A.W. kasema, “‘‘أُمِرْتُ أَنْ أُقَاتِلَ النَّاسَ حَتَّى يقولوا: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ ، وَيُقِيمُوا الصَّلاةَ ، وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ، فَإِذَا فَعَلُوا ذَلِكَ عَصَمُوا مِنِّي دِمَاءَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ إِلاَّ بِحَقِّ الإسْلامِ وَحِسَابُهُمْ عَلَى اللَّهِ’’Maana yake, “Nimeamrishwa (na Mwenyezi Mungu) nipigane na watu vita mpaka washuhudie kwamba hapana mungu anaepaswa kuabudiwa kwa haki ila ALLAH na MUHAMMAD ni Mtume Wake, na wasimamishe Sala, na watoe Zaka. Wakitenda hayo mambo watasalimika kwangu kutokana na uhai wao na mali yao isipokuwa kwa haki ya Uislamu. Na hisabu zao ni kwa Mwenyezi Mungu.”
Na pia katika Hadithi iliyopokelewa na Sayyidna Umar bin Khattaab R.A.A. na kutolewa na Baihaqi kasema, “Mtu mmoja alimuuliza Mtume S.A.W., “"يا رسول الله! أَيُّ الْعَمَلِ أَحَبُّ إِلَى اللَّهِ تعالى في الإسلام ؟ ، قال: الصَّلاةُ لوقتها ، ومن ترك الصَّلاة فلا دين له ، والصلاة عماد الدين"Maana yake, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Vitendo gani vinavyopendwa na Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Uislamu?” (Mtume S.A.W) akamjibu, “Sala katika wakati wake. Yeyote yule asiesali hana dini. Na Sala ni nguzo (ya pili) ya dini.”
Tena imetajwa watu wa aina tatu wasiokubaliwa Sala zao katika Hadithi iliyopokelewa na Abdallah bin L-`Aas R.A.A. na kutolewa na Abu Daud, Mtume S.A.W. kasema, “‘‘ثَلاثَةٌ لا يَقْبَلُ اللَّهُ صلاتهم: من تقدم قَوْمًا وَهُمْ لَهُ كَارِهُونَ ، وَمَنْ استعبد مُحَرَّرا ، وَرَجُلٌ أَتَى الصَّلاةَ دِبَارًا’’Maana yake, “(Aina ya watu) watatu ambao Sala zao hazikubaliwi na Mwenyezi Mungu, “Kiongozi anaechukiwa na raia zake; Mwuungwana ambaye anamtesa mtumwa wake baada ya kufanya mapatano naye kuwa atamwachia huru; na mtu ambaye hasali kwa wakati wake

No comments:
Post a Comment