Hii ni Sunna ya Udhu, na ni Sunna ya Mtume (Swallallahu Alaihi Wasallam), ambayo hupuuzwa na baadhi ya Waislamu.
Aishah (Radhiallahu Anha) amesimulia kuwa, Rasulullahi (Swallallahu Alaihi Wasallam) amesema; Rakaa mbili (za Swala zilizoswaliwa) baada ya kupiga Mswaki, ni bora mara sabiini kwa fadhila, kuliko rakaa sabiini (zilizoswaliwa) bila ya kupiga Mswaki.''
Imesemwa kwa mtu mwenyetabia ya kupiga Mswaki, hufa huku anaitamka ''Kalimah'' mwenye kutumia kasumba, ana hasara sabiini, moja kati yao; wakati wa kufa hawezi kuikumbuka '' Kalimah''
Katika Hadithi nyengine imesisitizwa sana kutumia Mswaki, na faida kumi zifuatazo;-
1. Huusafisha na kuutia utamu mdomo.
2. Ni sababu ya kumridhisha ALLAH (SW).
3. Na inamuudhi Iblisi.
4. ALLAH na Malaika wake humpenda mtu anayepiga Mswaki.
5. Hutia nguvu fizi na kuongeza nguvu za macho.
6. Huzuia nyongo na yabisi.
7. Huleta harufu nzuri mdomoni.
8. Huzidisha nuru ya macho.
9. Huondoa harufu mbaya mdomoni.
10. Na zaidi ya hapo ni Sunnah ya Mtume (Swallallahu Alaihi Wasallam).
Abu Khairah (Radhiallahu Anhu) amesema kuwa; ''Nilikuwa miungoni mwa ujumbe ambao ulikuja kwa Rasulullahi (Swallallahu Alaihi Wasallam), akatuzawadia mizizi ya Arak, ilituitumie kama miswaki, kwa hivyo tukamwambia; ''Ewe Rasulullah! Tunavyo (Vipande vya makuti vya mitende, kama miswaki), lakini tunaikubali Ikram yako, na zawadi yako.''
Abu Hurairah (Radhiallahu Anhu) amesimulia kuwa Rasullullahi (Swallallahu Alaihi Wasallam) amesema; ''Kama nisingelikuwa na hofu ya kuwatia mashaka Umma wangu, ningewaamrisha kupiga mswaki kwenye kila Swala.'' [Muslim]
MAELEZO;-
Mswaki ni ule mswaki wa asili, unaotokana na mizizi, au matawi ya miti tofauti. Mti unaojulikana zaidi, na wenye faida, ni ule wa mzizi wa Salvadora Persica. Mti wa jangwani, unajulikana kwa Kiarabu kama Arak, na kwa Kiurdu, Reelu.
Abu Ayoub (Radhiallahu Anhu) amesimulia kuwa Rasullullahi (Swallallahu Alaihi Wasallam) amesema; ''Mambo manne ni Sunnah za Mitume;-
1. Haya
2. Kutumia mafuta mazuri.
3. Kutumia Miswaki, na.
4. Ndoa.
Abu Umamah (Radhiallahu Anhu) amesimulia kuwa Rasullullahi (Swallallahu Alaihi Wasallam) amesema; ''Kila mara aliponijia Jibrili (Alaihisalamu) alinihimiza kutumia mswaki, mpaka nikahofia kuwa (kutokana na kutumia mswaki) ninaweza kuumiza ufizi wangu.
Insha-Allah, ALLAH atupe Tawfiq, ktk utekelezaji, ili tupate Ujira wa kutumia Mswaki, Amiin.

No comments:
Post a Comment