Thursday, June 28, 2012

TAHADHARI NA KUTELEZA KWA ULIMI


Ulimi ni kiungo muhimu katika mwili wa mwadamu. Ulimi ni neema kubwa miongoni mwa neema alizo neemeshwa mwanadamu na Allah (SW). Kiungo hiki ni silaha yenye makali mawili, silaha ya kusababisha mwanadamu  kufaulu hapa duniani na kesho Akhera, au nisilaha ya kumuangamiza mwanadamu hapa duniani na kesho akhera.

Kumcha Mwenyezi Mungu ni njia ya kuokoka duniani na kesho akhera Amesema Mwenyezi Mungu (SW):
قال تعالي : {ومن يتق الله يجعل له مخرجا و يرزقه من حيث لا يحتسب ومن يتوكل علي الله فهو حسبه إن الله بالغ أمره قد جعل الله لكل شئ قدرا}.
{{ Na anayemuogopa Mwenyezi Mungu humtengenezea njia ya kuokoka (na kila balaa). Na humpa riziki kwa namna asiyotizamia, na anayemtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtoshea. Kwa yakini Mwenyezi Mungu amekwisha kiweka kila kitu kipimo chake}}. Na Mwenyezi Mungu (SW) ni mjuzi wa kila kitu na hapitiwi na kitu chochote kilichoko mbinguni na ardhini. Tahadhari juu yetu kufanya jambo lisilomridhisha. Amesema Mwenyezi Mungu (SW) ushuhuda juu yaliopita:
وقوله : {وسع ربي كل شىء علما أفلا تتذكرون}
{{ Mola wangu anakijua vyema kila kitu. Basi je, hamsiki mawidha (hamzinduki)}}.
Ulimi ni neema aliompa Mwenyezi Mungu mja wake. Amesema Mwenyezi Mungu (SW):         قال تعالي : {ألم نجعل له عينين ولسانا وشفتين، وهديناه النجدين}
{{ Je hatukumpa macho mawili ? na Ulimi na Midomo miwili. Na tukambainishia zote njia mbili (iliyo njema na iliyo mbya) }}. Maiti wangapi wamesababisha vifo vyao kwa ajili ya ndimi zao. Je hawatatupwa watu motoni ispokuwa kwa mavuno ya ndimi zao. Inapasa kwa muumin kuhifadhi ulimi wake kwa hali yoyote ile na kujiepusha na kila ambalo linapingana na sheria, mfano wa kusengenya.  Amesema Mwenyezi Mungu (SW):
قال الله تعالي: {ولا يغتب بعضكم بعضا أيحب أحدكم أن يأكل لحم أخيه ميتا فكرهتموه}.
{{ Wala baadhi yenu wasiwasengenye wengine. Je Mmoja wenu anapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa? La, Hampendi}}.  Imepokewa na Barzah al-Aslamy Amesema Mtume (SAW):  [ Enyi mulioamini,  kwa ndimi zenu, wala imani haijaingia katika vifua vyenu musiwasengenye Waislamu, wala msichunguze aibu zao na mwenye kuchunguza aibu ya muislamu Mwenyezi Mungu atafunua aibu yake na kumfedhehesha mbele ya watu].

Kuhadharishwa juu ya Fitna:
 Hadith imepokewa na Ibn Abass kuwa Mtume (SAW) alipita katika makaburi mawili akasema: [ Maiti hawa wawili wanaadhibiwa wala hawaadhibiwi kwa jambo kubwa, mmoja wao alikuwa hatambi anapokojoa na mwengine alikuwa akieneza fitna].

Kutilia umhimu Mtume (SAW) kuhifadhi Ulimi
Kuhifadhi ulimi ndiko kumiliki kheri zote.  Amepokea hadithi Muaadh Ibn Jabal kuwa Mtume Mtume (SAW) Amesema: Je nisikujuze kwa mambo yote hayo zuia ulimi wko (chunga ulimi wako).  Akasema. Muaadh: Je tutahisabiwa kwa tunachukizungumza.  Mtume akashangaa na kumuambia:  Je hawatupwi watu motoni ila kwa mavuni ya ndimi zao”.  Na alikuwa Mtume (SAW) akiwahimiza bibi zake kujihifadhi na maneno yasiomridhisha Mwenyezi Mungu. Imepokewa na Aisha nimemuambia Mtume (SAW) tosheka na bibi Safia kwa jambi kadha na kadha akimaanisha ya kuwa ni mfupi Mtume akamuambia: [ umetamka neno ambalo kwamba likichanganywa na maji ya baharini litachanganyika].

Hali ya Waislamu Leo kupuuza kuhifadhi Ndimi Zao
Inapatikana katika hali zifuatazo:
1-    Maneno yasiokuwa na faida
2-    Kuingilia jambo lisilo kuhusu.
3-    Kuingilia heshima za Waislamu.
4-    Ulimi mchafu
5-    Kuomboleza katika msiba.

Ushuhuda wa mambo yaliopita amehutubu na akarefusha maneno yake mbele ya Umar akasema Umar kurefusha maneno ni ya shetani. Na imepokewa hadith kutoka kwa Abu Hureira, Mtume (SAW) Amesema: [ Muislamu bora ni yule asiyeingilia mambo ya watu, na kuingilia heshima za Waislamu ni katika sifa za wanafiki]. Amesema Mtume (SAW): [ Ni haramu kwa ndugu yako Muislamu damu yake, hishima yake na mali yake, muislamu ndugu yake ni muislamu hamdhulumu wala hamkhini na akashiria katika kifua chake taqwa ni kwenye moyo]. Maneno machafu yalioenea katika mujtamaa wa kiislamu leo huenda kuwa sababu kubwa ni vyombo vya habari.  Amesema Mtume (SAW): [ Hapana kitu kizito katika mizani siku ya kiyama kama tabia nzuri na Mwenyezi Mungu anachukia maneno mabaya].
Ama kuomboleza katika msiba ni jambo la kijahilia ambalo limekatazwa, na tumeamrishwa tusubiri pindi tu tunapopatikana na msiba. Mtume (SAW) alipita kwenye kaburi na akamuona mwanamke analia akamuambia muogope Mwenyezi Mungu na usubiri, mwanamke akajibu hujali kilichinisibu wala hakujua kwamba anayejibizana nae kuwa ni Mtume (SAW) kamwaambia hakika ya subra ni katika tukio la Mwanzo.

Tahadhari Kueneza Urongo kwa Watu
Imepokewa hadithi kutoka kwa Mtume (SAW) akisema: [ Tahadharini na mrongo, kwani urongo unapeleka kwa uovu, na uovu unapeleka mtu kunigia motoni, na mtu anasema urongo mpaka anaandikiwa mmbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni mrongo]. Na Akasema tena Mtume (SAW) : [ Urongo haufai hata kwa dhihaka]. Wala kuahidi mtu mototo wake wala asimtimizieAmesema Mwenyezi Mungu (SW)  kuamrisha waumini kuwa imara katika kupokea habari:
  قال الله تعالي: { يا أيها الذين آمنوا إن جاءكم فاسق بنبإ فتبينوا أن تصيبوا قوما بجهالة فتصبحوا على ما فعلتم نادمين}
{[ Enyi mlioamini, kama fasiki akikujieni na habari yoyote msimkubalie tu, bali pelelezeni kwanza, msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa wenye kujuta juu ya yale mliyoyatenda}}

Mwenyezi Mungu pamoja na Malaika wake wanaandika wanachozungumza mwanadamu. Na wao wanahifadhi amali zote za kheir na shari.  Amesema Mwenyezi Mungu (SW):
  قال الله تعالي: { وإن عليكم لحافظين, كراما كاتبين يعلمون ما تفعلون} 
{{ Na hakika juu yenu kuna wenye kuwatunza. Watukufu wenye kuandika. Wanayajua yote manayoyatenda}}. Na Neno lake Mwenyezi Mungu (SW):
  وقوله: {إذ يتلقى المتلقيان عن اليمين وعن الشمال قعيد, ما يلفظ من قول إلا لديه رقيب عتيد}.
 {{ Wanapopokea wapokeaji wawili, anayekaa kulini na anayekaa kushotoni. Hutoi kauli yoyote ispokuwa karibu naye yuko mngojeaji tayari (kuandika)}}.
Amepokea Abu Hureira kuwa Mtume (SAW) amesema: [ Kuwa Malaika wanapokezana usiku na mchana wakikutana katika swala ya alfajiri na al-asri, kisha wanakwenda wale walio kuwa ni wa usiku. Na mola akiwauliza naye akijua; mumewaacha vipi waja wangu? Wakijibu; tumewaacha wa kiswali na tukawajia hali ya kuwa wanaswali].

Wito wa Kuwajibika kwa Maneno Mazuri
Kuwajibika kwa maneno mazuri ni sababu ya kufaulu na kusamehewa madhambi na kupata radhi zake Mola kwa ajili hiyo anasema Mola:
قال الله: {يا أيها الذين آمنوا اتقوا الله وقولوا قولا سديدا.  يصلح لكم أعمالكم ويغفر لكم ذنوبكم ومن يطع الله ورسوله فقد فاز فوزا عظيما}.
 {{ Enyi mlioamini, Muogopeni Mwenyezi Mungu  na semeni maneno ya haki. atakutengenezeni vizuri vitendo vyenu na atakusemeheni madhambi yenu; Na anayemtii Mwenyezi Mungu  na Mtume wake, bila shaka amefanikiwa mafanikio makubwa}}.

Mwisho
Ndugu Waislamu, Ulimi nikiungo muhimu katika mwili wa mawnadamu. Na kikiwa kizuri basi mwili wote huwa mzuri. Nijukumu la kila Mislamu kuulinda ulimi wake kwa kutumia katika kuzungumza mambo ya kheri, kuamrisha mema na kukataza mabaya. Tukifanya hivyo, tutakuwa tumefaidika na neema ya ulimi, na kupata radhi za Allah (SW). Namuomba Mwenyezi Mungu asituhisabu kwa yale tulioyazungumza ikiwa ni ya makosa, na kutupa ujira kwa maneno mazuri tuliyoyasoma.

No comments:

Post a Comment

Twitter Bird Gadget