Mingoni mwa misingi ya kisheria ni kufunga mlango wa fitna. Na miongoni mwa Rehma za Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni kufunga mlango wa shari, basi mwenye kufungua mlango huo atapata madhambi.  Amesema mshairi:- Ikiwa mja hatovaa vazi la ucha Mungu, atakuwa uchi hata kama amevaa nguo. Na mja mwema ni yule amchaye Mola wake, wala hakuna ubora kwa anaye muasi Mola wake.
Ndugu Waislamu, Leo tunashuhudia wazi kabisa namana ya wanawake wanavyo dhihirisha mapambo yao, na kutovaa hijabu. Na bila shaka, kitendo hichi ni katika madhambi makubwa, na ni sababu ya kuteremshwa adhabu duniani, na kupata adhabu kali siku ya kiama.  Ndugu zangu  Waislamu,  kuweni na adabu ya Mwenyezi Mungu na mwalazimishe wake zenu kuvaa hijabu na kusitiri miili yao kama alivyo amrisha  Mwenyezi Mungu (SW) katika Qur’an tukufu. Amesema Mwenyezi Mungu (SW):
قال عز وجل : {يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ حَسْبُكَ اللَّهُ وَمَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِنْ جَلابِيبِهِنَّ ذَلِكَ أَدْنَى أَنْ يُعْرَفْنَ فَلا يُؤْذَيْنَ وَكَانَ اللَّهُ غَفُوراً رَحِيماً}
{{ Ewe Mtume, Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa Kiislamu, wajitermshie vizuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane kuwa ni watu wa heshima ili wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu}}.
Jukumu  la kila Muislamu kupiga vita Fitna ya Wanawake
Enyi Waislamu mcheni Mwenyezi Mungu na katazeni wanawake wenu na binti zenu kudhihirisha mapambo yao. Ni lazima kila Muislamu abebe jukumu la kuamrisha mema na kukataza mabaya. Kwani, tukiacha kufanya hivyo, tutalaaniwa na Mwenyezi Mungu (SW) kama walivyo laaniwa watu waliotangulia. Amesema Mtume (SAW): [ Watu wakiona uoavu na wasiukataze uovu huo huhofiwa kuwateremkia adhabu ya Mwenyezi Mungu].  Amesema Mwenyezi Mungu (SW ):
   قال عز وجل : { لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ بَنِي إِسْرائيلَ عَلَى لِسَانِ دَاوُدَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ذَلِكَ بِمَا عَصَوْا وَكَانُوا يَعْتَدُونَ كَانُوا لا يَتَنَاهَوْنَ عَنْ مُنْكَرٍ فَعَلُوهُ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ}
{{ Walilaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israil kwa ulimi wa Daudi na Isa bin Maryam. Hayo ni kwa sababu waliasi wakipindukia mipaka. Hawakuwa wenye kuzuiana (kukatazana) mambo mabaya waliyokuwa wakiyafanya. Uovu uiloje wa jambo hili waliokuwa wakilifanya}}. Na amesema Mtume (SAW):  [ Atakaye uona uovu na auzuie kwa mkono wake, asipoweza kwa ulimi wake, asipoweza kwa moyo wake na ni udhaifu wa imani].
Ndugu katika imani, Mwenyezi Mungu (SW) Amewaamrisha wanawake kuvaa hijabu na kubakia majumbani mwao, na kutolegeza sauti zao.  Amesema Mwenyezi Mungu (SW):
قال تعالى : {يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِنَ النِّسَاءِ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلاً مَعْرُوفاً وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الأُولَى وَأَقِمْنَ الصَّلاةَ وَآتِينَ الزَّكَاةَ وَأَطِعْنَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ}
{{ Enyi wake wa Mtume, nyinyi sikama yoyote tu katika wanawake wengine. Kama mnataka kumcha Mwenyezi Mungu, basi msiregeze sauti zenu ili asitamani mtu mwenye ugonjwa moyoni mwake, na semeni maneno mazuri. Na kaeni majumbani mwenu, wala msionyeshe mapambo yenu kama walivyo kuwa wakionyesha mapambo yao wanawake wa zama za ujahili}}.
Masharti ya Hijabu:
a)    Kufunika mwili wote ispokuwa uso
b)    Hjabu isiwe na mapambo juu yake
c)    Hijabu iwe nzito wala isiwe yenye kuonyesha mwili
d)    Hijabu iwe pana wala isiwe yenye kubana mwili
e)    Hijabu isiwe na manukato
f)     Hijabu isifanane na vazi la mwanamume
g)    Hijabu isifanane na vazi la makafiri
h)   Hijabu isiwe ni vazi lenye kujulikana
Ushuhuda wa masharti yaliopita, Amesema Mwenyezi Mungu (SW):
قال تعالى: (( يا أيها النبي قل للأزواجك وبناتك ونساء المؤمنين يدنين عليهن من جلابيبهن ذلك أدنى أن يعرفن فلا يؤذين. وكان الله غفورا رحيما  ))
{{ Ewe Mtume, Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa Kiislamu, wajitermshie uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane kuwa ni watu wa heshima ili wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu}}. Na Akasema tena Mwenyezi Mungu (SW):
 قال تعالى: (( وَقُلْ لِلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلاَّ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَى جُيُوبِهِنَّ  ))
{{ Na waambie Waislamu wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirishe mapambo yao ispokuwa yanayodhihirika. Na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao }}.
Amesema Mtume (SW): [ Watu wawili ni watu wa motoni, mmoja wao ni mwanamke aliyevaa nguo lakini yuko uchi]. Na akasema Mtume (SAW) [ Mwanamke yoyote atakaye jitia manukato na akapita mbele ya watu, ili watu wakasikie harufu ya mafuta yake, basi mwanamke huyo ni mzinifu].  Amesema tena Mtume (SAW): [ Amemlaani Mtume wa Mwenyezi Mungu mwanamke mwenye kuvaa vazi la mwanamume, na mwanamume mwenye kuvaa vazi la mwanamke]. Na amesema tena Mtume (SAW): [ Atakaye jifananisha na watu basi ni katika wao]. Na amesema tena Mtume (SAW): [ Atakae vaa  vazi la kujionyesha, Mwenyezi Mungu Atamvisha vazi  la udhalili siku ya kiyama].
Ndugu katika imani, ni wajibu juu kila mwanamume kuhakikisha masharti  ya  hijabu wakati anapo mnunuliya mke wake au binti yake vazi la kuvaa. Amesema Mtume (SAW): [ Nyinyi wote ni wachunga, na kila mmjo ataulizwa juu ya ailcho akikichunga]. Inatupasa kumuogopa Mola wetu na kutekeleza majukumu yetu kama alivyo tuamrisha Mwenyezi Mungu
Sababu ya Uharibifu wa Wanawake
Ndugu Waislamu, inajulikana wazi ya kuwa wanawake wa leo wamezidi kuonyesha umbile lao na mapambo yao.  Kuna sababu nyingi  ambazo zimechangia kupatikana uharibifu katika jamii. miongoni mwasababau  hizo ni:-- Mwanamke kukaa faragha na mwanamume ambaye si mahrimu yake. Amesema Mtume (SAW): [ Hawatokaa faragha mwanamke na mwanamume ispokuwa shetaani huwa watatu wao].
 - kusafiri peke yake. Amesema Mtume (SAW): [ Asisafiri mwanamke ispokuwa awe na mahrimu Yake( wasioruhusiwa kumuoa) Wala asikae faragha mwanamke na mwanamume].
 - Wanawake wakiislamu kujifananisha na wanawake wakikafiri. Amesema Mtume (SAW): [ Atakaye jifananisha na watu basi ni katika wao].
 
Wajibu wa Viongozi na Mahakimu na Wanavyoni
Enyi waja wa Mwenyezi Mungu,  mcheni Mola wenu na tahadharini kwa mambo aliyoyaharamisha, na saidianeni kwa mambo mema na musiache kwa mambo ya haki na kusubiri. Na jueni ya kuwa Mwenyezi Mungu atawalipa kwa mambo muliyoyafanya. Na inalazimu kwa viongozi wanyanja tofauti kutonyamaza katika kuondosha uoavu,  Imepokewa kutoka kwa Mtume (SAW) : [ Hakutumilizwa Nabii ispokuwa alikuwa na wafuasi na wenye kuchukuwa uongozi wake, kisha wakawapatia mgongo wote waliokuja baada yake, wanazungumza mambo wasiyoyafanya, na wafanya mambo wasiyoamrishwa, atakae pigana nao kwa mkono wake, basi huyo ni muumini.  Atakaye pigana nao kwa moyo wake basi huyo pia ni muumini, wala hakuna baadaya ya hapo chembe yoyote ya imani (mkono, ulimi na moyo)].
Wito kwa Wanawake Wakiislamu
-          Muogope Mwenyezi Mungu!  Ewe mototo wa kike
-          Muogope Mwenyezi Mungu! Mwenye kujipamba na kwenda sokoni
-          Muogope Mwenyezi Mungu!  Mwenye kuvaa hijabu kama pambo wala si kwa kujistiri
-          Muogope Mwenyezi Mungu! Kwa kile alichokukalifisha, amabapo mbingu na ardhi imekataa kubeba.
-          Muogope Mwenyezi Mungu!  Na hifadhi nafsi yako.
-          Muogope Mwenyezi Mungu!  Na kutangamana na wanaume na kutoka  bila ya mahrim
-          Muogope Mwenyezi Mungu! Ewe Mwenye kuingia kwa matibabu bila mahrim.
-          Muogope  Mwenyezi Mungu!  Ewe mwenye kuwalea watoto wako malezi ya wanyama.
-          Muogope Mwenyezi Mungu!  Ewe mwenye kujitia manukato.
-          Muogope Mwenyezi Mungu! Na mrejee katika uongofu, jua kama adhabu kali mbele ya Mwenyezi Mungu,  na dunia si makaazi.
 
Mwisho
Ndugu Waislamu, Na kariri tena kwa kuwakumbusha jukumu kubwa tulilo beba nalo ni kuwasimamia wanawake na kuwaamrisha mema na kuwakataza mabaya. Fitna kubwa leo ulimwenguni ni fitna ya wanawake, na maadui wanawtumia wanawake kama njia ya kufikia malengo yao. Jamii nyingi zimeharibikiwa kwasababu ya kuharibika mwanamke. Kwahivo, Nilazima kila Muislamu ajitolee kwa hali na mali kuwahifadhi wanwake katika jamii yetu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awahifadhi mabanati wakiislamu kutokana na vitimbi vya wenye kufanya vitimbi.Ewe Mwenyezi Mungu wakusanye wao katika imani na kuwapa peposiku ya akhera Mwenyezi Mungu sitiri aibu zetu na utuhifadhi mbele yetu, nyuma yetu na upande wa kulia na upande wa kushoto na juu yetu
No comments:
Post a Comment